Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wakali wa zamani..
FB_IMG_1532352215201.jpg
FB_IMG_1532352204167.jpg
FB_IMG_1532352284709.jpg
 
Kuwa na afya bora haitokani na kula nyama , pilau, chips , biriani , soseji, bugger, n.k, mafanikio ya afya bora inatokana na vitu vifuatavyo.

1.Angalia afya ya akili , kimwili na kiroho.

kuwa mwenye afya bora ni rahisi sana kuliko unavyofikiria wewe, haikuchukulii muda mwingi wala pesa nyingi , mfano usafi wako mwenyewe kimwili, usafi wa mazingira yako, mahusiano yako , ndoa yako ina amani, na je mahusiano yako na Mungu yakoje,

kuna watu hata kuoga wao wanaona kama adhabu , eti akiwa ameoga asubuhi , basi hata usiku haogi anaenda kulala hivyo hivyo, nguo nazo hata hafui anavaa mara mbili au tatu eti mpaka aone imechafuka. haendi kucheki hata kama anaumwa bali anameza dawa kwa kuwa tu ana maumivu ya kichwa . unaongeza sumu mwilini.
 
2.Mawazo yako yote yawe na afya.

kuna watu wawili tofauti , kuna mtu anaeishi na kuna mwingine haishi, ingawa wote wako hai. mawazo yakom yakiwa na afya kila siku utakuwa unatafuta naman ya kufanikiwa , na kama una mafanikio basi utatafuta kusonga mbele zaidi, lakini mtu ambae haishi yeye siku zote anawaza kushindwa kushindwa, hata haoni njia ya kupita ili akafanikiwe.

mawazo yenye afya hutafuta ni wapi nikawasaidie wenye mahitaji , wakati wenye mawazo yalikufa wanawaza namna gani nitaiba , nitadhulumu, nitadanganya na kuharibu watu.
 
3.Fanya mazoezi.



mazoezi yakusaidia kuwa mwenye afya na mwenye furaha na nguvu, utakuwa unajisikia vizuri kila siku. utaonekana mwenye amani . na wala hutachukua muda mrefu , dakika 20-30 zinakutosha kukupa changamoto kubwa ya mafanikio
 
4.Usichukulie mazoezi kama ndio yatakusaidia kupunguza mwili.



huwezi kuwa unakula kila chakula maadamu ni chakula na kufikiria kuwa kwa sababu unafanya mazoezi basi utapungua mwili au ndio utakuwa mwenye afya nzuri sio. utakuwa ni kichaa maana utafanya mazoezi ya nguvu lakini hutafanikiwa malengo yako.

fanya mazoezi kwa afya na huku ukiwa makini katika ulaji wako wa kila siku. njia hizi zitakusaidia.

_kula kila unaposikia njaa tu.

_ukiwa huna njaa usile.

_kunywa maji ya kutosha.

_lala masaa 7 usiku,

_fanya mazoezi kila siku.
 
5.usisikilize watu.

Ninaposema usikilize mtu , kuna watu wanapenda kukatisha watu tamaa , ukiwa umeamua kufanya kitu songa mbele bila ya kusikia ya watu. unaweza kusikiliza lakini unapima. kama yana akili.
 
6.Changamoto itakufanya utokezee mahali.

kama ukikutana na watu wenye mafanikio makubwa , wale wanaojulikana ulimwenguni , wamepitia changamoto nyingi na ngumu sana. na ni lazima uelewe hakuna mafanikio yanayokuja bila ya changamoto. . changamoto huleta mafanikio na mafanikio huleta changamoto. huwezi kufanikiwa ikiwa maisha ni rahisi .
 
7.JIULIZE KWA NINI. SWALI HILI NI KUBWA.

Unaweza kuwa unajiuliza kwa nini mimi , kwa nini yule, labda kwa sababu ya kuwa na afya nzuri kuliko wewe, au kuwa na maendeleo makubwa kuliko wewe. majibu unayo wewe , upande wangu naona kuwa kuna watu huchukua maamuzi magumu kuliko wengine huwa wanajihurumia na kuona kama aibu kufanya vitu ambavyo vinawaletea mafanikio.
 
8.Kumbuka kuwa kitasa kidogo kinafungua milango mikubwa na mageiti makubwa.



Unapoamua kufanya kitu kimoja kitasaidia vitu vingi, ukifanya maamuzi mazuri katika maisha yako, kila kitu kitakwenda vizuri, kitu kidogo utakachoanza nacho kitafungua mambo makubwa maishani.
 
8.Kumbuka kuwa kitasa kidogo kinafungua milango mikubwa na mageiti makubwa.



Unapoamua kufanya kitu kimoja kitasaidia vitu vingi, ukifanya maamuzi mazuri katika maisha yako, kila kitu kitakwenda vizuri, kitu kidogo utakachoanza nacho kitafungua mambo makubwa maishani.
 
Back
Top Bottom