Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

3.Fanya mazoezi.

mazoezi yakusaidia kuwa mwenye afya na mwenye furaha na nguvu, utakuwa unajisikia vizuri kila siku. utaonekana mwenye amani . na wala hutachukua muda mrefu , dakika 20-30 zinakutosha kukupa changamoto kubwa ya mafanikio
 
587862-8ad5c87860bcfc3f40c37b2954116f40.jpg
 
4.Usichukulie mazoezi kama ndio yatakusaidia kupunguza mwili.

huwezi kuwa unakula kila chakula maadamu ni chakula na kufikiria kuwa kwa sababu unafanya mazoezi basi utapungua mwili au ndio utakuwa mwenye afya nzuri sio. utakuwa ni kichaa maana utafanya mazoezi ya nguvu lakini hutafanikiwa malengo yako.

fanya mazoezi kwa afya na huku ukiwa makini katika ulaji wako wa kila siku. njia hizi zitakusaidia.

_kula kila unaposikia njaa tu.

_ukiwa huna njaa usile.

_kunywa maji ya kutosha.

_lala masaa 7 usiku,

_fanya mazoezi kila siku.
 
6.Changamoto itakufanya utokezee mahali.

kama ukikutana na watu wenye mafanikio makubwa , wale wanaojulikana ulimwenguni , wamepitia changamoto nyingi na ngumu sana. na ni lazima uelewe hakuna mafanikio yanayokuja bila ya changamoto. . changamoto huleta mafanikio na mafanikio huleta changamoto. huwezi kufanikiwa ikiwa maisha ni rahisi .
 
7.JIULIZE KWA NINI. SWALI HILI NI KUBWA.

Unaweza kuwa unajiuliza kwa nini mimi , kwa nini yule, labda kwa sababu ya kuwa na afya nzuri kuliko wewe, au kuwa na maendeleo makubwa kuliko wewe. majibu unayo wewe , upande wangu naona kuwa kuna watu huchukua maamuzi magumu kuliko wengine huwa wanajihurumia na kuona kama aibu kufanya vitu ambavyo vinawaletea mafanikio.
 
8.Kumbuka kuwa kitasa kidogo kinafungua milango mikubwa na mageiti makubwa.

Unapoamua kufanya kitu kimoja kitasaidia vitu vingi, ukifanya maamuzi mazuri katika maisha yako, kila kitu kitakwenda vizuri, kitu kidogo utakachoanza nacho kitafungua mambo makubwa maishani.
 
10.Unastahili kuwa na afya bora.

kwa nini uteseke kwa kwa sababu tu ya vitu vinavyovutia macho , chips zinavutia sana , nyama za kuchoma, pombe, sigara, na vyakula vingi vya kukaanga. unaweza kula lakini ule kwa adabu , sio kwa fujo. wenye afya wana uchaguzi. chagua vyakula vyenye akili hata kama una hela nyingi kula vyakula vyenye akili vipo . isile mradi unakula.
 
11.Kila asubuhi panga miango yako ya siku.

Kila siku ikiwa unapanga mipango yako na kuhakikisha unafanya yote, ingawa kuna ambayo hutafanikisha lakini kwa sehemu kubwa utafanya. utaona mafanikio yako na kutimiza ndoto yako.
 
12.Uwe mwoga.

Utapataje kitu bila msukumo , kitu kinachoonekana ni kigumu na hakina hata njia ya kufanya kinaogopesha, lakini kinakufanya uondoke katika kiti chako na kukifanya kwa sababu ya kuogopa kupoteza. na kwa kuwa unatafuta kufanikiwa lazima ule woga utakufanya uondoke.
 
CHAKULA NA DAWA.

Ilikuwa vigumu kufikiria muda nguvu utulivu na pesa ambayo nilitumia kutafuta uponyaji na afya njema na amani .ilikuweka afya yangu vizuri kila wakati nilijaribu kitu kipya cha kunisaidia kiafya ,mara mazoezi na jinsi kuwa vizuri ,nilichanganyikiwa katika kuchunguza namna ya ulaji mbalimbali na namna tofauti tofauti.

NILIKUWA NA MATUMAINI NA KUPATA KITABU KIMOJA CHA KUNISAIDIA AU UTARATIBU WOWOTE AMBAO UNGENISAIDIA BILA YA KUHARIBU MAISHA YANGU

Hii ni baada ya kugundua kitu gani kinafanya kazi vizuri. watu wengi pia wamekuwa wakikumbana na matatizo kama yangu ya kutafuta afya na kuishi kwa na afya njema.

kwa nini kuna kuwa na watu au makundi mengi yanahangaikia kutafuta maamuzi na kutafuta majibu ,pia watu wa wa bidhaa za afya pia nao kwa nini wapo kwetu ? ni kwa sababu wengi wetu tu wagonjwa , tumechoka,na tuna misongo ya maisha ,kabla hata ya wakati .
 
Back
Top Bottom