Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Unaweza kusema mpango wa mabasi ya abiria katika mikoa ya Dar es Salaam na Arusha kuanza safari za ndani na nje ya nchi saa 11 alfajiri kuanzia leo Oktoba 9, 2018 umekwama.

Oktoba 5, 2018 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye amesema safari hizo zilitarajiwa kuanza mapema lakini kuna masuala yaliyokuwa yanashughulikiwa na Sumatra na kubainisha kuwa zitaanza leo.

Mikoa mingine ambayo mpango inatekeleza mpango huo ni Mbeya, Mwanza na Dodoma.
 
MCL Digital leo lilitembelea vituo vya mabasi vya jijini Dar es Salaam na Arusha na kushuhudia mabasi hayo yakiondoka muda wa kawaida wa saa 12 asubuhi badala ya saa 11 alfajiri.

Katika jiji la Arusha, mabasi mengi yaliondoka saa 12:10 kutokana na ukaguzi uliokuwa unafanywa na jeshi la polisi.

John Laizer mkazi wa Sakina Arusha, alisema kuwa alifika kituo cha mabasi saa 10:45 alfajiri akitegemea kuondoka mapema saa 11 lakini alikwama.
 
wanasema bado taratibu lakini mbona serikali ilitangaza leo, nadhani kuna tatizo"alisema

Jijini Dar es Salaam, MCL Digital lilifika kituo kikuu cha mabasi ya mikoani cha Ubungo (UBT) na kushuhudiwa mabasi hayo yakiondoka saa 12 tofauti na agizo Nditiye aliyetaka yaondoke saa 11 kuanzia leo.

Mmoja wa karani wa basi la kampuni ya Simba, Juma Ally alisema imeshindikana kwa kuwa maandalizi hayajakamilika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…