1. Mlo
Vitu unavyokula vina mchango mkubwa katika ngozi na afya yako kwa ujumla. Ili kupata ngozi nzuri iliyo laini, nyororo na inayong'aa inabidi uache vyakula na vinywaji vinavyotengenezwa viwandani, wanga, mafuta na sukari na badala yake kula protini, matunda, mboga na kunywa maji kwa wingi.
Hakikisha unakunywa maji si chini ya glasi nane kwa siku na matunda pamoja na mboga kila unapopata mlo.
Matunda na mboga za matawi husaidia oksijeni kuzunguka vizuri mwilini na kwenye ngozi kuliko mafuta au kipodozi chochote unachoweza kupaka.
Protini husaidia kujenga ulinzi zaidi katika seli za ngozi ambayo ngozi inahitaji kukabiliana na ukavu wa ngozi. Nayo maji husaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini na kusaidia vinyweleo kupumua vizuri, hivyo kuzuia bakteria chini ya ngozi.