Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mara nyingi ni vigumu kukumbuka ni aina gani ya chakula ambacho kina saidia sehemu mbalimbali za mwili. kuna vyakula vinavyofanana na hizo sehemu za mwili ambavyo vitakufanya ukumbuke kuvinunua kwa faida ya mwili wako.

Angalia hizi sehemu 5 ambazo zinaonekana sawasawa kabisa na hizo sehemu. na utahakikisha kuwa ni kweli
 
Figiri Mwitu Na Mifupa.



Mashina ya hio mboga ya figiri huonekana kama mifupa , kama uonavyo hapo, mboga ya figiri ina sodiamu inayosaidia kuimarisha mifupa, ukiwa unakula hii mboga inaziba nafasi ilio haribika kwenye mfupa na inakuwa na nguvu ya kutosha.
 
Karoti Na Macho.



Kipande cha karoti kinakumbusha jicho lako, rangi ya chungwa ya karoti inayotokana na mmea wenye chemical ya beta carotene inayosaidia kuondoa mtoto wa jicho , inasaidia kukuza misuli ya kwenye jicho na seli kuzorota, na hii inatokea sana ukifikia miaka ya 50 na kuendelea.

linda macho yako kwa kutumia karoti za kutosha .
 
3.Mvinyo Mwekundu, na Damu.



Zabibu Na DAMU.



Mvinyo mwekundu una antioxidants na una polyphenols za kutosha, na unaonekana kama damu, mvinyo mwekundu au red wine ina uwezo wa kuzuia na kupunguza kutoka kwa damu nyingi unapokatwa na kitu.
 
4. Viazi vitamu Na Kongosho.



Viazi vitamu huonekana kama kongosho, vinasaidia kukuza viungo kwenye mwili, viazi vina beta carotene nyingi zinazolinda tissue za kongosho ili kuepukana na madhara ya saratani ukiwa mtu mzima wakati huo. kula viazi vitamu mara kwa mara ili vikulinde na madhara hayo.
 
5.Walnuts na Ubongo.



Inashangaza kuona vyakula baadhi jinsi vinavyofanana na sehemu ya mwili , kama walnut inafanana kabisa na ubongo wa human being. inasaidia mikunjo na kasoro kwenye mwonekano , imekusanya Omega 3, fatty acid inayotegemeza afya ya ubongo ili kufanya kazi vizuri na pia ina vitamini E.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…