Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Man City inashika nafasi ya pili katika msimamo wa kundi F, ikiwa na pointi tatu moja nyuma ya vinara Lyon ya Ufaransa ambayo leo itachuana na Hoffenheim ya Ujerumani.
Akifafanua Guardiola alisema ili kutwaa taji hilo panahitajia nguvu na msukumo kutoka kwa kila mmoja kuanzia wachezaji, kocha, viongozi na mashabiki pia jambo ambalo kwa sasa halipo ndani ya City.
Kocha huyo alitwaa mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiinoa Barcelona ya Hispania lakini hakufanya hivyo alipoiona Bayern Munich.
 
Mechi zote za Ligi ya Mabingwa Ulaya zitakazopigwa leo ni AEK Athens vs Bayern Munich, Young Boys vs Valencia, Ajax vs Benfica, Hoffenheim vs Lyon, Manchester United vs Juventus, Real Madrid vs FC Viktoria Plzen, AS Roma vs CSKA Moscow na Shakhtar Donetsk vs Manchester City.
 
Klabu ya Chelsea imempiga tafu kiungo wake wa zamani Frank Lampard, ambaye kwa sasa ni kocha wa Derby County FC imemruhusu kumtumia mchezaji Mason Mount katika mchezo baina ya timu hizo mbili wa michuano ya Kombe la Ligi.
Chelsea imeiruhusu klabu hiyo kumtumia kiungo huyo katika mechi ya raundi ya nne ya mashindano hayo baina ya timu hizo itakayochezwa Oktoba 31 mwaka huu kwenye uwanja wa Stamford Bridge.
Kanuni za chama cha soka England inazuia mchezaji anayecheza kwa mkopo kucheza dhidi ya timu yake aliyotokea ila kwa idhini ya klabu husika kama ilivyofanya Chelsea.
 
Hata hivyo uamuzi wa Chelsea kumruhusu Mason Mount, 19 kucheza dhidi yao unaonekana kama kumbeba au kumtunzia heshima Lampard, ambaye alidumu Stamford Bridge kwa miaka 13 kuanzia 2001–2014 akicheza mechi 429 na kufunga mabao 147.
Mbali ya kumruhusu Mount pia Chelsea imeiruhusu Derby kumtumia mlinzi kinda asiyekuwa na namba ya kudumu kwenye klabu hiyo, Fikayo Tomori mzaliwa wa Canada aliyebadili uraia na kuchagua kuitumikia timu ya Taifa ya England.
Ingawa mlinzi huyo hakucheza lakini Mount alikuwa kwenye kikosi cha Derby kilichoiadhiri Man United katika raundi ya tatu kwenye uwanja wa Old Trafford na kiwango bora alichonacho kwa sasa kimemshawishi kocha wa timu ya Taifa ya England, Gareth Southgate kumuita kwenye kikosi chake.
 
Katika taarifa iliyotolewa na klabu hiyo na kutumwa kwenye chama cha soka na bodi ya ligi, Chelsea ilisema imetoa Baraka zote wka Derby kuwatumia wachezaji hao katika mchezo huo wa raundi ya nne wa kombe la Ligi.
“Chelsea FC inapenda kutangaza leo kwamba imeiruhusu Derby County kuwatumia wachezaji wawili wanaocheza huko kwa mkopo Mason Mount na Fikayo Tomori katika mechi ya raundi ya nne ya ‘Carabao Cup’,” ilisema taarifa hiyo.
 
Nyota wa Juventus, Cristiano Ronaldo ameitambulisha saa ya gharama ambayo imetengenezwa kwa vito vya thamani, baada ya kuonyesha wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Saa hiyo ya gharama ilitambulisha jana Jumatatu ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo utaoikutanisha Juventus dhidi ya Manchester United mechi ambayo inatarajiwa kuwa na ushindiani mkali kutokana na ubora wa timu hizo.
 
Jose Mourinho ametamka wazi kwamba mchezaji wake Anthony Martial ajiandae kwenye kikosi cha kwanza kitakachoanza katika mchezo dhidi ya Juventus leo Jumanne usiku.

Miamba hiyo ya soka ya Italia itakuwa na kibarua kigumu ambapo Man United iakuwa ikijaribu kulinda heshima kwenye uwanja wake wa nyumbani, Old Trafford.

Tayari Jose Mourinho ameanza kutangaza silaha zake za kuimaliza Juventus baada ya kumweleza Martial kuwa ataanza kwenye kikosi cha leo usiku dhidi ya Juventus.
 
Nyota huyo anashuka dimbani kuikabili Juventus huku akiwa na rekodi nzuri ya mchezo uliopita ambapo aliiwezesha timu yake kupata mabao mawili ambayo yote aliyatupia wavuni, walipokutana na Chelsea Jumamosi wiki iliyopita.

Hata hivyo mabao hayo yakarudishwa na wapinzani wao huku Ross Barkley akiisawazishia timu yake bao la usiku na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2
 
Hii inaweza kuwa ni habari mbaya kwa Kocha wa Real Madrid, Julen Lopetegue baada ya kuwapo tetesi kuwa huenda Antonio Conte akarithi mikoba yake.

Miamba hiyo ya soka barani Ulaya imepoteza michezo yake ya mwisho minne kati ya mechi tano.

Pia Real Madrid inakamata nafasi ya saba kwenye msimamo wa La Liga baada ya juzi Jumapili kupoteza mchezo wake ilipokutana na dhidi ya Levante mechi ambao iliiisha kwa Real Madrid kuzamishwa mabao 2-1.
 
Kutokana na mfululizo wa matokeo hayo mabaya, tayari kumekuwa na minong’ong’ono kuwa huenda Conte akarithi mikoba ya kocha huyo kipindi cha kiangazi.

Matokeo mabaya ya Jumapili yameiweka pabaya Real Madrid kuelekea mchezo dhidi ya mahasimu wao Barcelona Jumapili wiki ijayo.

Kwa mijibu wa Gazeti la The Mirror, hadi sasa Conte ndiye kocha pekee anayetajwa kuwa ana asilimia kubwa kuchukua mikoba ya Popetegui ambaye kibarua chake ni hatihati kuendelea.
 
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, atamkosa mshambuliaji wake mahiri Alexis Sanchez katika mchezo wa leo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Juventus.
Sanchez aliumia na kupumzishwa katika mchezo uliopita dhidi ya Chelsea, uliochezwa Jumamosi iliyopita na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2, ambapo Mourinho amesema anakosekana katika mchezo muhimu.
Mchezo huo wa leo utachezwa kwenye Uwanja wa Old Trafford na unaweza kuwa mbaya kwa Mourinho iwapo vijana wake watashindwa kumdhibiti mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo Cristiano Ronaldo anayeitumikia Juventus akitokea Real Madrid.
 
Mourinho alisema ingawa wanatamani kupata ushindi, lakini anakubaliana na ushauri wa matabibu wa klabu hiyo kutomtumia Sanchez aliyejitonesha kifundo cha Jumamosi iliyopita na nyota huyo anayelipwa mshahara mkubwa wa Pauni 500,000 kwa wiki, atakuwa nje kwa kipindi cha wiki mbili hadi tatu.
Mshambuliaji huyo alimkuna Mourinho alipofunga bao la ushindi walipoishinda Newcastle United kwa mabao 3-2 likiwa ni bao lake la kwanza tangu Aprili alipofungwa bao la ushindi katika nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Tottenham.
Akiuzungumzia mchezo huo wa Mourinho, alisema ni mtihani mkubwa kwake kwani mbali ya Sanchez pia atawakosa wachezaji wengine kadhaa ambao ni majeruhi.
Aliwataja baadhi ya wachezaji anaotarajia kuwakosa kuwa ni pamoja na Marouane Fellaini, Victor Lindelof, Diogo Dalot, Scott McTominay na mshambuliaji kinda wa Uingereza, Jesse Lingard.
Kukosekana kwao kwenye mazoezi ya timu hiyo kwenye uwanja wao wa Carrington jana Jumatatu kunamaanisha kuwa kocha huyo atawapanga Anthony Martial, Juan Mata na Marcus Rashford kumsaidia Romelu Lukaku katika safu ya ushambuliaji.
Man United iliyoanza ligi hiyo vizuri ikiishindilia Young Boys ya Uswisi kwa mabao 3-0 ikiwa ugenini ilibanwa na Valencia katika mechi yake ya pili na kulazimishwa sare ya 0-0 kwenye uwanja wa Old Trafford.
Mchezo wa leo ni mtihani mwingine kwa Mourinho, ikizingatiwa kuwa Juventus haijapoteza mechi yoyote msimu huu na katika Ligi Kuu Italia na ligi ya Mabingwa ilianza kwa kuichapa Valencia 2-0 ugenini kabla ya kuinyuka Young Boys 3-0.
Pengine sare ya mabao 2-2 iliyopiata Man United mbele ya Chelsea Jumamosi iliyopita itaipa nguvu ya kuondoka na ushindi leo mbele ya Juventus inayoongozwa na Ronaldo, mshambuliaji wa zamani ‘Mashetani wekundu hao’.
 
Back
Top Bottom