Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Klabu za Wolves, Leicester City, Southampton na Fulham zinahusishwa na harakati za kumsajili kiungo wa Ureno Joao Mario. Mario,25, hajacheza hata mechi moja katika klabu ya Inter Milan msimu huu. (Calciomercato)
 
Juventus na Borussia Dortmund ni miongoni mwa klabu kubwa ambazo wanamfuatilia kiungo kinda wa Uingereza Matt O'Riley,17, anayekipiga katika klabu ya Fulham. (Evening Standard)
 
Kocha wa Manchester United Jose Mourinho anahofia kumpoteza golikipa wake kutoka Spain David De Gea 27 ambaye anaweza kuhamia Juventus, wakati ambapo mkataba wake utaisha msimu ujao wa kiangazi. (Irish Sun)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…