Msanii wa muziki wa Dansi kutoka Tanzania, Johnson Nguza ‘Papii Kocha' ametoa taarifa kuwa amepata mtoto. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Staa huyo wa wimbo wa 'waambie' aliweka Video fupi iliyoonesha sura ya mtoto na kuandika, "Mungu ni Mwema karibu Mwanangu". _ Hata hivyo Mbali na taarifa hizi zake za kupata mtoto, haijabainika nani mama wa mtoto huyo kwakuwa Papii amekuwa ni msiri juu ya mahusiano yake kwa kipindi chote tangu arudi uraiani. Papii ana mtoto wa kike aitwaye Aisha ambaye tayari ameshaingia katika umri wa utu uzima.