DEREVA WA BASI LA HEKIMA ZA MUNGU MATATANI KWA KUFANYA MAKOSA MBELE YA WAZIRI LUGOLA - Gari lililokuwa limembeba Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, limenusurika kugongwa na basi la Kampuni ya Hekima za Mungu - Dereva wa basi hilo alitaka kulipita gari la Waziri Lugola katika eneo lilisoruhusiwa kisheria. Tukio hili limetokea mchana wa leo Wilayani Gairo Mkoani Morogoro - Baada ya basi hilo kupita Waziri Lugola alimuagiza dereva wake alifuatilie na baada ya kulikuta dereva wake alikaguliwa na kubainika hana sifa za udereva - Waziri Lugola aliagiza dereva huyo akamatwe atakapowafikisha abiria wa basi hilo.