Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mke wa Mchungaji, Kanisa la Last Church Lusajo Mwambene amekutwa amejinyonga kwa kamba ndani ya Kanisa hilo huku sababu zikiwa hazijulikani, inaripotiwa kuwa mwanamke huyo alifiwa na kichanga chake na alikuwa akienda makaburini mara kadhaa na baade hakuonekana tena
 
Kiungo wa Manchester City, Kevin de Bruyne, ameumia goti lake la kushoto kwenye mechi ya Carabao Cup jana dhidi ya Fulham. Kocha wa klabu hiyo, Pep Guardiola amesema De Bruyne atafanyiwa uchunguzi na madaktari na watakuja na majibu.
 
India yazindua sanamu ya aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu wa kwanza wa nchi hiyo Sardar Patel , ambayo imekuwa sanamu ndefu zaidi duniani yenye mita 182. Baadhi ya wananchi walalamika kuwa jambo hilo ni ufujaji wa pesa zao za kodi.
 
Msanii wa muziki nchini Marekani Kanye West ‘YE’ amesema anajiweka mbali na masuala ya kisiasa baada ya kukiri kuwa alikuwa anatumika kueneza jumbe zenye chuki bila idhini yake, kupitia ukurasa wa twitter amesema sasa anaanza kufanya mambo yake ya ubunifu zaidi.
 
Aliyempa mimba dada yake miaka 30 jela || . Mkazi wa kijiji cha Usagara wilayani hapa Mkoa wa Mwanza, Charles Abel (24) amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa makosa mawili ya kubaka na kumpa mimba mwanafunzi wa darasa la saba wa Shule ya Msingi Busagara.
 
Back
Top Bottom