Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tofauti na maeneo mengine ya nchi ambapo mwanaume ndio hutoa posa kwa familia ya mwanamke, utamaduni huu mpya unawashinikiza wasichana kumlipa pesa mwanamume.
Inasadikiwa kuwa pesa hizo ni kama dola 1500 na huongezeka kulingana na uwezo wa familia ya msichana.
Waliyoshuhudia wanasema pesa hizo lazima zipatikane kwa udi na uvumba.
 
Tofauti na maeneo mengine ya nchi ambapo mwanaume ndio hutoa posa kwa familia ya mwanamke, utamaduni huu mpya unawashinikiza wasichana kumlipa pesa mwanamume.
Inasadikiwa kuwa pesa hizo ni kama dola 1500 na huongezeka kulingana na uwezo wa familia ya msichana.
Waliyoshuhudia wanasema pesa hizo lazima zipatikane kwa udi na uvumba.
 
Lakini ni nini kinacho wafanya vijana kugeuza utamaduni uliopo?
Katika tamaduni za wanyarwanda mahari lazima itolewe tena na bwana harusi mtarajiwa.
Hata kama mahari haijakamilika kwa wakati huo familia husika zinakubaliana jinsi itakavylipwa, na hatimae harusi hufanyika
Katika mkoa wa msgharibu nchini Rwanda pesa hizo zikikosekana hakuna harusi tena.
 
Kaibanda Bernard ameiambia BBC kuwa vijana "Wanafanya hivyo wakisema idadi ya wasichana sasa hivi ni kubwa sana''
Wasichana wengine wameshindwa kuvumilia, ambapo msichana akitinga umri wa miaka kumi na tano hivi anatafuta pesa kwa nguvu ili aweze kumnunua bwana.
Vijana wenyewe wanaona ni ishara ya ushirikiano katika familia mpya kutokana na hali ya maisha ilivyo ghali siku hizi.
 
John Gatera anasema mmoja wa watu wanaounga mkono mtindo huo wa maisha anasema "Zamani kutoa mahari ilikuwa ni kitu rahisi sana ni ngombe labda na kiwanja lakini sasa hata kupalilia sehemu ya ujenzi lazima ulipe pesa''.
Anasema yeye binafsi akifikisha umri wa kuoa lazima msichana amlipe pesa la sivyo harusi haitafanyika.
Baadhi ya watu katika kijiji cha Nyamashekhe wanataka serikali kuingilia kati suala hilo.
Mmoja wao ni mzee Kaihura ambaye anasema''Kijana hawezi kupata heshima katika jamii ikiwa hatatoa mahari''.
 
Utamaduni huu mpya umepokelewaje?
Wazazi waliyo na mabinti waliyofikisha umri wa kuolewa wana wasisi huenda mtido huo mpya wa maisha ukaenea kote nchini ikiwa hatua hazitachukuliwa kuukomesha
 
Pia wanahofia suala hili huenda likabadilisha kabisha utamaduni wa jadi wa wanaume kulipa mahari.
Vijana hususana katika mkoa huo wanadaiwa kujiona ''mastaa'' hali ambayo huenda ikawafanya kuzembea majukumu yao ya familia hata wakifanikiwa kupata mwake zao.
 
Sio mara ya kwanza Mkoa huo wa Magharibi ambao ndio mkubwa kuliko mikoa mingine kuzua gumzo kuhusiana na masuala ya kijamii.
Kabla ya mtinduu huu wa sasa wa vijana kutaka walipwe pesa na wasichana ili wawaoe, kulikuwa na wakati inadaiwa kuwa mvulana akimtembelea mchumba wake kwao sharti achinjiwe kuku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…