Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Vita itakuwa kwenye timu hizo sita kuwania nafasi nne. Hakuna anayependa kucheza kwenye Europa League. Wote wanataka kucheza kwenye michuano yenye hadhi kubwa, Ligi ya Mabingwa Ulaya. Hapo ndipo inapokuja ile methali ya kwamba mwenye kisu kikali ndiye anayekula nyama. Man United wanaonekana kuikaribia kasi yao, huku kocha Jose Mourinho akionekana kuanza kupata huduma nzuri kutoka kwa Luke Shaw na Anthony Martial.
 
Lakini, huko kwenye kikosi cha Arsenal, kocha Unai Emery, naye anaonekana kuanza kuipata huduma nzuri ya Granit Xhaka na Alexandre Lacazette. Huko kwa Maurizio Sarri, Alvaro Morata amerudi kwenye makali yake ya kufunga mabao huku Mauricio Pochettino na Jurgen Klopp wakifanya vyema na vikosi vyao vya Spurs na Liverpool. Pep Guardiola na Man City yake ndiye anaonekana kuwa na uhakika wa kwamba hawezi kukosekana kwenye ile Top Four.
 
IMG-20181106-WA0070~2.jpeg
 
Shughuli kwa hawa wababe wengine, nani atapenya na nani atashindwa? Tofauti ya pointi baina ya vigogo hao sita ni ni tisa, lakini kuna tofauti ya pointi nne baina ya timu inayoshika nafasi ya nne na ile ya saba, ambao ni Man United. Lakini, Man City yenyewe imezizidi timu zinazoshika namba mbili na tatu, Chelsea na Liverpool pointi mbili tu. Hiyo ina maana kama Man City watashindwa kuifunga Man United kwenye mechi ijayo, kisha Liverpool au Chelsea zikashinda mechi zao, msimamo utakuwa tofauti kabisa.
 
Huu ndio ukweli unaoifanya Ligi Kuu England hasa kwa wale vigogo wa Top Six kila mmoja acheze kama fainali ili asipoteze. Kupoteza kwa sasa hakuruhusiwi na ndio maana Man United walipambana kugeuza matokeo ya kufungwa na Bournemouth na kushinda ili kuendelea kuwamo kwenye vita hiyo. Ndio maana Arsenal waligoma kupoteza mbele ya Liverpool. Hupaswi kupoteza, ukipoteza unapotezwa
 
Ni kipindi kizuri cha kuona ufundi wa makocha na hicho ndicho kitakacholeta tofauti. Ni wakati wa Mourinho kuonyesha kwanini yeye ni Special One, lakini makocha wengne pia wakiwa na kazi ya kuthibitisha kwamba hawajakosea kuwamo kwenye vikosi hivyo vinavyohesabika kuwa ni timu kubwa zaidi kwenye ligi hiyo. Nani atabaki? Hivi ndivyo Top Four inavyoleta raha kuliko mbio za ubingwa wenyewe kwenye ligi hiyo.
 
ARSENAL wanachekelea wanachokiona kwa sasa katika timu yao. Lakini Rio Ferdinand, mlinzi wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya England amedai kwamba anajua sababu ya msingi ambayo inawafanya Arsenal wachekelee.
 
Jumamosi jioni, Arsenal walionyesha kiwango bora katika pambano la Ligi Kuu ya England dhidi ya Liverpool ambalo walitazamiwa kufanya vibaya kutokana na ukali wa Liverpool licha ya siku za karibuni kushinda mechi nyingi mfululizo.
 
Ferdinand anaamini kwamba licha ya wachezaji wengi wa Arsenal kuwa vizuri lakini ni mchezaji mmoja tu ndiye ambaye amesababisha kwa kiwango kikubwa mambo kwenda sawa pale Arsenal. Lucas Torreira, staa wa kimataifa wa Uruguay.
 
Torreira ambaye ni mfupi kwa kimo, alinunuliwa kwa dau la pauni 25 milioni kutoka Sampdoria ya Italia katika dirisha kubwa lililopita mara baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la dunia nchini Russia ambako alikuwa akiiwakilisha Russia.
 
Amekuwa mchezaji wa kudumu katika kikosi cha Arsenal kwa sasa na katika pambano dhidi ya Liverpool, Torreira alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi na Arsenal haijapoteza pambano lolote katika mechi ambao yeye ameanza msiu huu.
 
Ferdinand anaamini kwamba staa huyo ndiye chachu ya kila kitu katika kikosi cha Arsenal na kwa muda mrefu walikuwa wakikosa mchezaji wa aina yake katika kikosi cha Arsenal ambacho kilikuwa kinasuasua katika utawala wa kocha aliyepita, Arsene Wenger.
 
Kitu kikubwa kwa Torreira ni kwamba anaijua nafasi yake. Arsenal wameleta wachezaji wengi katika nafasi yake kwa miaka mingi lakini wote walichemsha. Torreira ni aina ya mchezaji ambaye anaweza kuifungua safu ya ulinzi kwa pasi. Atacheza pasi fupi kwa ajili ya kuiendesha timu.” alisema Rio.
 
anataka kuchukua mpira ili kuwawezesha wachezaji wengine kama akina Mesut Ozil kucheza. Anaweza kuilinda safu ya ulinzi na hilo ni jukumu kubwa kwa timu ambayo inataka kushambulia.” Alisema Ferdinand ambaye kwa sasa ni mchambuzi mahiri wa soka England.
 
Kitu kikubwa kwa Torreira ni kwamba anaijua nafasi yake. Arsenal wameleta wachezaji wengi katika nafasi yake kwa miaka mingi lakini wote walichemsha. Torreira ni aina ya mchezaji ambaye anaweza kuifungua safu ya ulinzi kwa pasi. Atacheza pasi fupi kwa ajili ya kuiendesha timu.” alisema Rio.
 
anataka kuchukua mpira ili kuwawezesha wachezaji wengine kama akina Mesut Ozil kucheza. Anaweza kuilinda safu ya ulinzi na hilo ni jukumu kubwa kwa timu ambayo inataka kushambulia.” Alisema Ferdinand ambaye kwa sasa ni mchambuzi mahiri wa soka England.
 
Naye mlinzi wa zamani wa Arsenal, Martin Keown amekoshwa na kiwango cha staa huyo kwa jinsi ambavyo anaulinda ukuta wa ulinzi wa Arsenal kama ambavyo viungo wa enzi zao walikuwa wanafanya kwa ajili ya kuisaidia kazi safu ya ulinzi.
 
Back
Top Bottom