Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

491B8CB1-8B8D-4FFA-9BF6-F085A76E1DA3.jpeg
 
Punguza mwendo
Kila wakati unatakiwa kukumbuka ya kwamba Mwendokasi unaua, Mwendo mkubwa ni hatari sana, lakini ni hatari zaidi mara hali ya hewa inapokuwa mbaya. Kumbuka kuwa wakati wa mvua au ukungu barabara huteleza na ni vigumu kuona njia vyema.
 
2. Washa taa pale mvua au ukungu unapozidi.
Mara nyingi mvua pamoja na ukungu hukufanya ushindwe kuona barabara vyema. Hivyo ni muhimu kuwasha taa za ukungu (fog lights) mara zinapokuwa na umuhimu; inashauriwa kuwasha taa hizi ikiwa hauwezi kuona mita 100 mbele.
 
Usikaribie gari jingine sana.
Kwasababu ya kutokuona vyema pamoja na utelezi wakati wa mvua au ukungu, inashauriwa kutokulikaribia gari lingine sana.Hili litakuepushia kugongana na gari lingine kunapotokea swala kama vile gari kuteleza au kurudi nyuma ghafla
 
Pia ni vigumu kutambua kama mahali unapotaka kupita pana korongo au daraja limevunjika, kwani maji huwa yamefunika eneo husika.
Ni vyema kusubiri maji yapungue au yakauke kabisa ndipo upite kwenye eneo hili ili kuepuka ajali.
 
Kagua gari kabla ya safari
Kabla ya safari yoyote, gari kama chombo cha moto linahitaji kuandaliwa. Ni muhimu kuhakikisha taa, breki, injini, visafisha vioo (wiper blades), pamoja na sehemu nyingine za gari zinafanya kazi vyema kabla ya safari.
Kwa mfano utahitaji taa pamoja na visafisha vioo unapoendesha gari wakati wa mvua au ukungu ili uone mbele vyema. Hivyo swala la ukaguzi wa gari kabla ya safari haliepukiki.
 
Back
Top Bottom