Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Furaha ni kitu ambacho hakishikiki. Furaha unaweza kuipata pale unapoamua wewe binafsi. Furaha hutafutwa na mhusika mwenyewe. Furaha ni utulivu ulio ndani ya nafsi ya mtu (Binadamu). Msingi wa Furaha ni utulivu wa Mwili na Roho.
 
Utulivu wa mwili na roho unatengeneza matumaini na upendo uliomo ndani ya nafsi. Msingi wa furaha ni Upendo, au Mapenzi ya Mtu. Kupuuzia, kudharau, kusahau na kusamehe, kupenda huongeza nafasi ya kupata furaha ya moyo.
 
Tumshukuru Mungu kwa kila jambo linalotokea katika maisha yetu ya kila siku, na tusione kama Mungu hatupendi. Ukipata tatizo sema hili limekuja na mengine kumi yaje nipo tayari kuyapokea. Cheka then songa mbele na maisha yako.
 
Hivyo ili uwe na furaha ni lazima kukaa na watu wanaokupa furaha. Na fanya mambo yanayokupa furaha, . Watu wengi wanakosa furaha na amani na kujaa na msongo wa mawazo katika maisha yao ya kila siku hasa makazini, majumbani, kifamilia nk.
 
Watu wengi wanamalizia muda wao mwingi katika shughuli zao za kila siku kama vile , maofini, shuleni, vyuoni nk. Endapo maeneo haya mtu anakosa furaha ni mwanzo wa msongo wa mawazo, magonjwa, mwili kuchakaa nk. Tafuta chanzo cha tatizo ni nini, kama kuna uwezekano wa kuongea na viongozi wako, zungumza ili kutatua tatizo linalokunyima raha. Katika utafiti nilioufanya nimegundua kuwa viongozi wa idara mbalimbali wanaongoza kwa kukosa furaha katika shughuli zao za kila siku. Wanaishi kwa stress!!!
 
Tujaribu kufanyia kazi matatizo yetu yanayotukabili na kuchukua hatua asap, bila hivyo hutapata suluhu ya kitu kinachokunyima furaha!!!!!!!!!!!!!!!!!!Usiruhusu mtu ausononeshe moyo wako!! I always believe that my happiness is everything in my life.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…