Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Stewart Downing (20)

Mmoja kati ya viungo wawili kutokea katika orodha hii. Msimu wa 2011/12, Downing anajulikana kwa kucheza msimu mzima bila ya kufunga wala kutoa pasi ya bao wakati huo akicheza mechi 36 za Ligi Kuu ya England na Liverpool. Bahati mbaya zaidi kwake aligongesha besela mara 20. Tunadhani hakuwa na bahati tu.
 
Fernando Torres (21)

Mmoja kati ya wafungaji bora katika Ligi Kuu ya England hasa akiwa na Liverpool kabla ya nuksi kumuingia akiwa na chelsea. Kama alivyokuwa hatari katika kuziona nyavu basi ndivyo hivyo hivyo ambavyo staa huyu wa Hispania anayekipiga Japan kwa sasa ndivyo alivyokuwa hatari katika kuzikosa nyavu. Aliondoka zake England akiwa amegongesha besela mara 21.
 
Sergio Aguero (21)

Mwingine ambaye hajamalizana na miamba ni huyu hapa staa wa kimataifa wa Argentina. Bado anakipiga Manchester akiwa ni mfungaji bora wa muda wote klabuni hapo.

Angeweza kuwa na idadi ya mabao mengi zaidi kama mashuti yake 21 yaliyogonga miamba yangeingia kwa ndani kidogo.
 
Peter Crouch (22)

Kwa urefu wake sijui wakati mwingine anashindwa nini kuinamisha kichwa chake na kukandamiza mpira kwa chini. Crouch ambaye amecheza timu mbalimbali za Ligi Kuu ya England zikiwemo Tottenham, Portsmouth, Liverpool na Stoke City ni miongoni mwa mastaa ambao wamegonga besela mara nyingi zaidi katika Ligi Kuu ya England. Mara 22.
 
Jermain Defoe (23)

Unafahamu kwamba Defoe amegonga mwamba mara nyingi kuliko pasi alizowapasia wenzake ndani ya eneo la adui? Hapana shaka ubinafsi huu wakati mwingine unamfanya akose bahati ya kufunga baadhi ya mabao. Amegonga besela mara 23. Na bado kwa sasa anakipiga Bournemouth kwa hiyo anaweza kuendelea kuigonga miamba zaidi.
 
Luis Suarez (26)

Wakati akiwa katika misimu yake ya mwisho Anfield, staa huyu mng’ataji wa kimataifa wa Uruguay alikuwa hashikiki kwa kuziona nyavu. Lakini kumbe alikuwa hashikiki kwa kuzikosa nyavu vile vile. Ndani ya msimu mitatu na nusu tu aliyokaa England aligonga besela mara 26. Msimu wa 2013/14, Suarez alifikia rekodi ya kufunga mabao mengi ndani ya msimu mmoja wakati alipofunga mabao 31. Hata hivyo msimu huo pia aligongesha besela mara tisa na angeweza kufikisha mabao 4.
 
Steven Gerrard (26)

Aliiacha Ligi Kuu ya England akikumbukwa kwa upambanaji wake kama nahodha wa Liverpool. Lakini akaiacha Ligi akikumbukwa kama mmoja kati ya wachezaji waliokuwa hodari katika kupiga mashuti ya nguvu. Kwa kipindi kirefu alichotamba katika Ligi Kuu ya England Gerrard alijulikana sana kwa kupiga mashuti makali.

Mengi yaliwaweka kiroho papo mashabiki wa timu pinzani kutokana kugonga besela. Alipiga mashuti 26 yaliyogonga besela.
 
Wayne Rooney (29)

Kama mashuti ya Rooney ambayo yamegonga besela yangeingia katika nyavu basi si ajabu Rooney angekuwa amebakisha mabao machache tu kufikia rekodi ya Alan Shearer ambaye ni mfungaji bora wa muda wote katika Ligi Kuu ya England.

Hata hivyo bado ni ngumu kuthibitisha hilo kwa sababu katika rekodi za Opta bado hatujajua Shearer naye angefikisha mabao mangapi kama mashuti yake yaliyogonga mwamba yangeingia katika nyavu. Bado hatuna uhakika sana.
 
Robin van Persie (44)

Tofauti kati ya RVP na mchezaji aliyeshika nafasi ya pili, Rooney ni kubwa kuliko tofauti ya Rooney na mchezaji aliyeshika nafasi ya nane. Hii inakuonyesha ni jinsi gani RVP alikuwa anakumbwa na tatizo la kukosa mabao mara nyingi uwanjan
 
Kama mashuti ya staa huyu wa kimataifa wa Uholanzi aliyestaafu soka hivi karibuni akiwa na timu yake ya utotoni, Feneyoord yangekuwa yanaingia katika nyavu hapana shaka angekuwa mfungaji bora wa sita wa muda wote katika Ligi Kuu ya England mbele kidogo ya mkali wa Liverpool, Robbie Fowler. Amekuwa na mafanikio na Man United, akiwa na mabao 144 mpaka sasa anashika nafasi ya 11.
 
Fernando Torres (21)

Mmoja kati ya wafungaji bora katika Ligi Kuu ya England hasa akiwa na Liverpool kabla ya nuksi kumuingia akiwa na chelsea. Kama alivyokuwa hatari katika kuziona nyavu basi ndivyo hivyo hivyo ambavyo staa huyu wa Hispania anayekipiga Japan kwa sasa ndivyo alivyokuwa hatari katika kuzikosa nyavu. Aliondoka zake England akiwa amegongesha besela mara 21.
 
FB_IMG_1539296587018.jpg
 
Back
Top Bottom