Fernando Torres (21)
Mmoja kati ya wafungaji bora katika Ligi Kuu ya England hasa akiwa na Liverpool kabla ya nuksi kumuingia akiwa na chelsea. Kama alivyokuwa hatari katika kuziona nyavu basi ndivyo hivyo hivyo ambavyo staa huyu wa Hispania anayekipiga Japan kwa sasa ndivyo alivyokuwa hatari katika kuzikosa nyavu. Aliondoka zake England akiwa amegongesha besela mara 21.