Anaitwa Farid Qubanda ni mzaliwa wa mkoa wa Mwanza, wengi wanamfahamu kwa jina la Fid Q ambali ndio jina lake la kisanii. Nguli huyu wa music wa Hip Hop Bongo anajulikana pia kama mkali wa mashairi kutokana na uwezo wake mkubwa alionao katika masuala mazima ya uandishi bora wa mashairi, watu wengine wamefikia sehemu wanamuita Genius.
Ndani ya miaka ya 2017 na 2018 ata ikiokea Fi Q mwenyewe akasema ulikua ni miaka bora au wenye mafanikio kwake ila kutakua na ukweli usiopingika kua pia ulikua ni miaka mibaya kwa upande wake.
Nimesema hivyo kutokana na kwamba wengi tunafahamu vita kali inayoendelea duniani kwa sasa ni vita ya mitandao hasa mitandao ya kijamii, watu wamekua wakifanya mambo ya ajabu na kubwa zaidi ni migogoro inayopelekea watu kutupiana lugha mbaya yaani matusi.
Fid Q amekua ni mmoja ya wasanii waliokumbana na hili balaa ndani ya hii miaka, hii imechangiwa na yeye kujikuta ameingia/ameingizwa katikati baina ya pande mbili zinazo lumbana na yeye kuonekana kuegemea upande mmoja labda kwa yeye kujua au kutokujua.
Mitandaoni kumekua na makundi mbali mbali (teams) yanayotofautiana kutokana na mapenzi juu ya vitu vinavyotofautiana hivyo basi watu wamekaa tayari wakisubiri mtu ujichanganye tu. Kuna msemo unasema "nikanyage bahati mbaya nikulipue makusudi" basi hayo ndio yalimkuta Fid Q baada ya kutoa wimbo wake uitwao Fresh ambao aliutolea tena Remix baada ya kuombwa na msanii Diamond, hivyo ilikua ni Fresh remix - Fid Q ft Diamond.
Inshu hapa haikua Fresh remix wala haikua Fid Q ft Diamond bali inshu ilikua ni mashairi ya Diamond ndani ya huu wimbo. Mashairi ya Diamond yalionekana moja kwa moja kua ni madongo kwenda kwa hasimu wake mkubwa hapa bongo ambae si mwingine bali ni Ali K au Alikiba wengi wanamuita King Kiba.
Hapo juu nimeeleza jinsi mambo mitandaoni ya navyokua, Sasa basi baada ya huu wimbo kutoka tu ndio Fid Q alijikuta kawakanyaga bahati mbaya Team Kiba na wao wakaanza kumlipua makusudi, sababu ni kwamba waliona kua katumika katika huu mchongo wa kumchafua msanii wao wanaomuhusudu kupita kiasi.
Richa ya FID mwenyewe kukanusha kua hakujua kitu chochote yeye alifanya tu kama wimbo kawaida na alitumia neno "nilifichiwa white" lakini kama nilivyokuambia hapo juu jamaa anajulikana kama genius hivyo basi wadau walimwambia kama wewe ni kichwa mbona umezidiwa ujanja na kujikuta ukitumika?. Zaidi ilikua ni matusi tu na kejeli aliyo ambulia mitandaoni na kwingine kote.
Hii hali ilionekana kumuumiza sana Fid Q mpaka akaamua kwenda studio na kutoa ngoma (Kiberiti - Fid Q ft Saida Karoli) iliyotokana na hii inshu, kama nilivyokupasha habari hapo juu jamaa ni mkali wa mashairi na ana uwezo mkubwa katika hili swala hivyo alichokifanya ni kuchukua baadhi ya madongo na kejeli alizopewa kipindi cha huu mkasa na kuyabadirisha kuwa mashairi.
Clouds vs Wasafi..
Siku sio nyingi zimepita tunajua nini kilikua kinaendelea katika mambo ya burudani hapa nchini, ni mvutano baina ya pande mbili tajwa hapo juu na uwanja wa mapambano ni kule kule kwenye mitandao ya kijamii.
Fid Q kwenye mdomo wa Mamba kwa mara nyingine
Hii ni baada ya yeye kutoa kauli uliyoonekana kama dongo kwa upande fulani(Wasafi). Inawezekana alitoa kauli akiwa na nia nzuri tu lakini wadau hawahitaji kulijua hilo wao wanasubiri ujichanganye tu ili wakuvuruge sawa sawa.Yaliyomkuta mwaka jana kwa teamKiba ndio yaliyomkuta mwaka huu kwa teamWasafi na matawi yake yote wakiwemo na viongozi, sio kingine bali ni kejeli na matusi ya hapa na pale.
Mtazamo wangu
Haya yote yaliyomtokea yanaweza kua na faida na hasara kwa Fid, kama ilivyo game ya sasa imekua ikiendeshwa na kitu wanaita Kiki hivyo basi haya yanawezakua ni kiki kwa jamaa ikafanya kufatiliwa na kuongelewa sana.
Lakini nikiangalia upande wa pili sioni kama ni sahihi kwa kiki za hali hii ya kudhalilishwa na kutukanwa mitandaoni kama tujuavyo heshima inachukua muda sana kuijenga lakini ni swala la sekunde kadhaa tu kuishusha sasa hii inaweza kupelekea kushuka kwa heshima yake kwani amekua ni mmoja wa wasanii hapa bongo wenye heshima kubwa.
Kua makinini bro, kua kama Prof J bro
Mimi naitwa Davet