Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Johannesburg, Afrika Kusini. Ofisa mmoja wa polisi ambaye hakuwa kazini Jumatatu alifyatua risasi katika Mahakama iliyokuwa ikisikiliza shauri la talaka yake na akamuua mkewe aliyetengana naye na kaka wa mkewe wakati wa mapumziko.

Mkasa huo ulitokea katika mahakama ya hakimu mkazi iliyoko ghorofa ya nane kwenye mji wa bandari wa Durban ulioko Kusini mwa Afrika Kusini.
 
Muda was aa 5:00 asubuhi mtuhumiwa alimpiga risasi mkewe na kaka wa mkewe na wote wawili walikufa papo hapo,” msemaji wa polisi Kanali Thembeka Mbele aliiambia AFP na akaongeza kwamba usikilizaji wa kesi hiyo ulikuwa unakaribia kuanza baada ya mapumziko ya chai. Kisha mtuhumiwa mwenye umri wa miaka 32 alijigeuzia bunduki ili ajiue lakini hakufa."

"Alijaribu kujiua, akachukuliwa na kupelekwa hospitalini akiwa mahututi,” alisema.
 
Mbele alithibitisha kwamba mtuhumiwa huyo hakuwa kazini siku hiyo na vyombo vya habari vinasema marehemu walikuwa mahakamani hapo wakati muuaji alipowafuata na kuonyesha kama alitaka kuzungumza nao kabla ya kuwafyatulia risasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…