Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

PAUL Pogba wa ndani ya uwanja kwa msimu huu huwezi kumweka daraja moja na mastaa kama Cristiano Ronaldo na Lionel Messi. Lakini, inapokuja suala la pesa, staa huyo wa Ufaransa anacheza kwenye ligi moja na wakali hao.
 
Kwa mujibu wa Forbes kuhusu mapato ya wanasoka waliovuna kwa mwaka huu, Pogba anashika namba tano kwenye orodha ya mastaa wenye mkwanja mrefu, lakini akiwa mchezaji pekee wa kutoka Ligi Kuu England aliyeingia kwenye anga hizo za wakali kama Ronaldo, Messi na Neymar.
 
Forbes limefanya majumlisho ya mishahara na bonasi za wachezaji na malipo mengine ya wadhamini na kupata kiwango cha pesa ambazo wanasoka wamevuna kwa mwaka mzima, ndipo ilipopatikana orodha hiyo ya wakali watano na hii ndiyo orodha kamili.
 
5.Paul Pogba -Dola 29.5 milioni

Mambo ya kisoka ya kiungo Paul Pogba huko Manchester United si mazuri. Lakini, mambo ya kipesa yapo vizuri kutokana na Mfaransa huyo kuingiza kipato cha Dola 29.5 milioni mwaka huu kutokana na Jarida la Forbes. Pogba amevuna Dola 25 milioni kama mishahara na bonasi zake anazolipwa huko Old Trafford, wakati Dola 4.5 milioni alizivuna kupitia dili zake za kibiashara. Wadhamini wakubwa wa Pogba ni Adidas, ambao wamekuwa wakifanya naye dili tamu staa huyo na kumfanya kuwa kwenye orodha hiyo ya wanasoka wanaopiga pesa nyingi kwa mwaka huu. Hata wakati Pogba anahama kutoka Juventus kwenda Man United kwa ada ya Pauni 89 milioni, Adidas ndio waliofichua dili hilo kupitia tangazo lao.
 
Pogba anakuwa mchezaji pekee kutoka kwenye Ligi Kuu England ambaye mwaka huu amekuwa na kipato kikubwa kwenye orodha ya wanasoka waliokunja pesa nyingi kwa mujibu wa jarida hilo maarufu la masuala ya kipesa.
 
4.Gareth Bale - Dola 34.6 milioni

Staa wa Real Madrid, Gareth Bale naye ameingia kwenye orodha ya wanasoka waliovuna pesa nyingi kwa mwaka huu baada ya kuweka kibindoni Dola 34.6 milioni.

Bale anavuna Dola 28.6 milioni kutoka kwenye mkataba wake anaolipwa huko Real Madrid, huku dili zake za kibiashara zimemwingizia Dola 6 milioni. Kama ilivyo kwa Paul Pogba, Bale naye wadhamini wake ni Adidas na ndio mastaa wao wakubwa wanaofanya vizuri kwenye soka la Ulaya.
 
3.Neymar -Dola 90 milioni

Supastaa wa Kibrazili, Neymar haishangazi kuwapo kwenye orodha hii. Staa huyo alihama Barcelona kwenda Paris Saint-Germain kwa ada ya Euro 222 milioni majira ya kiangazi mwaka jana wakati wababe hao wa Ufaransa waliponunua mkataba wake huko Nou Camp. Kwa mujibu wa Forbes, Neymar amevuna kipato cha Dola 90 milioni mwa mwaka huu, ikiwa ni zaidi ya mara mbili ya kiwango alichovuna staa wa Real Madrid na Wales, Gareth Bale. Hata hivyo, kwa kiwango hicho cha Neymar kinafanya kuwapo kwa pengo kubwa sana la kipato kati ya mastaa watatu wa juu, ambapo Mbrazili huyo ameachwa kwa mbali na, Ronaldo na Messi.
 
Neymar analipwa mishahara na bonasi nyingine, Dola 73 milioni, wakati dili zake za kibiashara anavuna Dola 17 milioni. Baadhi ya kampuni zinazofanya kazi na staa huyo ni Nike, Red Bull, Gillette, Beats by Dre na McDonald’s.
 
2.Cristiano Ronaldo - Dola 108 milioni

Supastaa Cristiano Ronaldo anashika namba mbili kwenye orodha ya wanasoka matajiri kutokana na kipato chake cha mwaka huu kilichobainishwa na Jarida la Forbes.
 
Kwa sasa, Ronaldo anayekipiga Juventus na huko ameonyesha umahiri wake wa kutikisa nyavu kwenye Serie A. Ronaldo anavuna Dola 108 milioni na tofauti ya Ronaldo na Lionel Messi ipo kwenye dili zao za kibiashara. Ronaldo mishahara yake na bonasi ni Dola 61 milioni, wakati dili zake za kibiashara anavuna Dola 47 milioni.
 
Kwenye suala la kuwa nembo ya biashara, Ronaldo yupo juu ya Messi, lakini Muargentina huyo anapiga pesa ndefu kupitia mishahara yake anayolipwa huko Nou Camp. Kwa mwaka huu, Messi ndiye staa mwenye kipato kikubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…