Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

STAA wa zamani wa Leicester City na Tottenham, Gary Lineker amemwambia kiungo N’Golo Kante aihame tu Chelsea kwa sababu Kocha Maurizio Sarri haeleweki.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekuwa akicheza vyema kabisa kiungo ya kukaba, lakini kwa sasa Sarri amekuwa akimtumia kwenye kiungo ya kushambulia kitu ambacho kinaharibu kabisa uwezo wa mchezaji huyo.
Kocha Sarri anaona ni vyema kumtumia Jorginho staa wake aliyetoka naye Napoli kwenye kiungo huyo ya kukaba.
 
Lakini, Lineker amemwambia Kante aihame tu The Blues kama ataendelea kuchezeshwa kwenye nafasi asiyoweza kuimudu. Mwanasoka huyo wa zamni wa England alisema Kante hawezi kukosa timu za kucheza na kama akiwa tayari timu nyingi tu zinaingia vitani kuwania huduma yake.
Bahati mbaya ni kwamba Kante alisaini mkataba mpya hivi karibuni wa kuendelea kubaki Stamford Bridge.
 
Lineker alituma picha na kuandika maneno yalikuwa na kichwa hiki cha habari: “Sarri: Kante sio Jorginho.”
Kisha kwenye mtandao wa Twitter aliandika: “Sawa, amepewa mkataba mpya, lakini kwa hili jambo linaloendelea, haitashangaza kama kutakuwa na timu nyingine kuja kutaka saini yake.”
Sarri alidai mchezaji wake anayetaka kumchezesha kwenye kiungo ya kukaba, anapenda awe fundi wa mpira, hivyo kwenye kikosi chake ni Jorginho au Cesc Fabregas ndio wanaofaa kucheza kwenye eneo hilo na si Kante.
 
Mwandishi wa habari mmoja mwenye uhusiano mzuri sana na Man United, Duncan Castles alisema staa huyo wa kimataifa wa Chile ameumia na hivyo atakuwa nje ya uwanja pengine inaweza kuwa kwa mwezi mzima, ikiwa ni kipindi muhimu sana kwa timu hiyo kuwa na huduma ya mchezaji huyo kwenye Ligi Kuu England.
 
Hata hivyo, kumekuwa na taarifa nyingine zinazodai mchezaji huyo anaweza kuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili.
Kama lisemwalo lipo na kisha Sanchez akawa nje ya uwanja kwa mwezi mzima, basi jambo hilo litamfanya akose mechi nane, ikiwamo dhidi ya Arsenal, timu yake ya zamani na Liverpool uwanjani Anfield. Mechi nyingine kubwa atakayokosa ni ile ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ya kukamilisha hatua ya makundi dhidi ya Valencia.
 
Hata hivyo, jambo hilo limekuwa pigo hata kwa Sanchez mwenyewe ambaye alitaka kutumia mwezi huu wa Desemba kuonyesha kiwango bora kabisa ili kuzivutia timu nyingine hususani Paris Saint-Germain ili kuja kumsajili dirisha la Januari. Kama Sanchez atakuwa kweli mgonjwa na kuwa nje ya uwanja kwa mwezi mzima, hii ndio orodha ya mechi atakazokosa.
 
Hata hivyo, jambo hilo limekuwa pigo hata kwa Sanchez mwenyewe ambaye alitaka kutumia mwezi huu wa Desemba kuonyesha kiwango bora kabisa ili kuzivutia timu nyingine hususani Paris Saint-Germain ili kuja kumsajili dirisha la Januari. Kama Sanchez atakuwa kweli mgonjwa na kuwa nje ya uwanja kwa mwezi mzima, hii ndio orodha ya mechi atakazokosa.
 
Southampton – ugenini (Desemba 1)
Arsenal – nyumbani (Desemba 5)
Fulham – nyumbani (Desemba 8)
Valencia – ugenini (Desemba 12)
Liverpool – ugenini (Desemba 16)
Cardiff – ugenini (Desemba 22)
Huddersfield – nyumbani (Desemba 26)
Bournemouth – nyumbani (Desemba 30)
 
Back
Top Bottom