Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

WAKALA wa supastaa Gareth Bale, Jonathan Barnett amefunguka na kusema mteja wake anaweza kutimkia Italia siku za baadaye baada ya kuona Real Madrid wamekuwa hawaeleweki.
Staa huyo wa kimataifa wa Wales amekuwa na msimu mgumu huko Bernabeu, akishindwa kuziba pengo lililoachwa na Cristiano Ronaldo kwenye kikosi hicho baada ya kutimkia zake Juventus dirisha lililopita la usajili wa majira ya kiangazi.
 
Ukweli, Bale ameshindwa kucheza kwa kiwango bora kile kilichowashawishi Real Madrid kutoa pesa ndefu kumsajili wakati huo akitokea Tottenham ya Ligi Kuu England.
Kwa hali ilivyo, kwa sasa kama Bale ataamua kuachana na Real Madrid, basi halitakuwa jambo la kushtua, huku ripoti zikidai akiamua kurudi England basi mahali anakotaka kwenda ni Manchester United pekee.
Man United wanaweza kuchangamkia saini yake baada ya Alexis Sanchez kushindwa kufanya kile wanachohitaji, huku makinda Anthony Martial na Marcus Rashford wakiwa na viwango vinavyobadilikabadilika kama homa za vipindi.
 
Lakini, Man United hawataki kukurupuka kumsajili mchezaji huyo na ndio maana wakala wake amekuwa akizungumza uwezekano wa kwenda Italia.
"Kwenda kucheza Italia? Kwa sasa bado anafurahia maisha ya Madrid, lakini kwa kipindi cha huko baadaye hakuna kisichowezekana," alisema Barnett.
 
HAPA mwenye kisu kikali ndiye atakayekula nyama. Linalosemwa ni kwamba supastaa wa Kibrazili, Neymar ana makubaliano na klabu yake ya Paris Saint-Germain kwamba kama kutakuwa na timu itakayokuwa na pesa inayoanzia Euro 200 milioni na inahitaji saini yake, basi asiwekewe kizuizi, wamuuze tu.
 
Kama hilo ndilo, basi kwa hali ya soka ilivyo kwa sasa kuna timu kibao zinaweza kuonyesha jeuri ya kunasa huduma ya mchezaji huyo. Kwa dau hilo la Euro 200 milioni, Neymar hawezi kubaki PSG zaidi ya msimu huu. PSG wenyewe walimnasa mwaka jana tu hapo kwa ada ya Euro 222 milioni wakati waliponunua mkataba wa mchezaji huyo kama kipengele kilivyokuwa kikielezwa na wababe wa Nou Camp, Barcelona.
 
Kumeelezwa kwamba jambo hilo la kwamba Neymar anapatikana limezifanya klabu vigogo wa Ulaya kuanza kucheki uwezekano wa kumsajili.
Timu zenye pesa zinazotosha kummudu Neymar kwa maana ya usajili wake pamoja na mishahara watakayolazimika kumlipa kila wiki ni pamoja na Real Madrid, Manchester City, Manchester United, Chelsea, Juventus na Barcelona wenyewe.
 
Ripoti zinadai kwamba rais wa Real Madrid, Florentino Perez mpango wake ni kumnasa staa huyo, ambaye Real Madrid ilikuwa ikimsaka tangu alipokuwa Santos ya Brazil. Barca nao wamedaiwa wanataka kuingia vitani kumrudisha staa wao huyo wa zamani ili kwenda kurudisha makali katika kikosi chao. Jambo hilo litaibua vita upya huko kwenye La Liga kwa Real Madrid na Barcelona kugombea huduma ya Neymar. Lakini, huko kwenye Ligi Kuu England, kuna vigogo watatu wanaotajwa kwamba watachuana jino kwa jina kumsaka Mbrazili huyo.
 
Man City ya Pep Guardiola itaongoza vita hiyo sambamba na Man United ya Jose Mourinho huku Chelsea ya Maurizio Sarri pia wakidaiwa kwamba wanaweza kuingia kutetemesha. Juventus wanajaribu kujitengeza ili kuja kuteka soka la Ulaya na jambo hilo liliwafanya kumnasa Cristiano Ronaldo kwenye dirisha lililopita, hivyo haitaonekana ajabu kama itaingia sokoni kumsaka Neymar, ambaye aliwahi kukiri kwamba soka la Italia linaanza kumvutia upya baada ya CR7 kutua Turin.
 
Hili la vigogo wenye pesa kila mmoja kuanza kumtolea macho Neymar ndilo linalotoa ishara kwamba kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi, kutakuwa na vuta nikuvute ya kuwania saini ya supastaa huyo wa Kibrazili.
 
Back
Top Bottom