Jambo hili linajadilika. Iwapo litawezekana, nitafurahi sana. Likishindikana (zikabadi timu 32) , vilevile itakuwa sawa tu. Jambo jema ni walau nitakuwa nimejaribu kulisukuma.
“Iwapo jambo hili linasaidia kuboresha soka, itakuwa vema zaidi. Iwapo madhara yake kwa usitawi wa eneo hilo yataonekana kuwa makubwa, basi liachwe.
Kuhusu uwezekano wa Saudi Arabia kuwa mwenyeji mwenza wa michuano, Infantino alisema: “Lazima tulitazame katika muktadha wa hali ya kisiasa katika eneo husika, tukitarajia mambo yatakuwa yameimarika na kuwa bora zaidi kwa ajili ya soka na dunia kijumla. Iwapo mjadala wowote kuhusu jambo hili utaimarisha ustawi katika ukanda huu, hasa kuhusu Saudi Arabia, litakuwa jambo jema sana.