Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

NAKWAMBIA Jose Mourinho shughuli anayo. Kikosi chake cha Manchester United kimemaliza nafasi ya pili kwenye kundi lake katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na jambo hilo linamweka kwenye hatari ya kupangiwa vigogo wa maana kwenye hatua ya mtoano ya 16.
 
Timu zote nne za Ligi Kuu England zimefuzu kutinga hiyo ya mtoano, lakini kwa Manchester City inayonolewa na Pep Guardiola mambo yake yanaonekana kuwa na unafuu kutokana na timu anazoweza kupangiwa nazo kutokuwa tishio sana.
 
Man United iliyomaliza nyuma ya Juventus kwenye kundi lake, inaweza kupangwa na Real Madrid, Bayern Munich, Barcelona, PSG, Borussia Dortmund na FC Porto sawa na itakavyoweza kupangiwa Liverpool ya Jurgen Klopp isipokuwa PSG tu ambayo ilipangwa kwenye kundi moja.
 
Spurs inayonolewa na Mauricio Pochettino inaweza kupangiwa na Real Madrid, Bayern Munich, Juventus, PSG, Dortmund na FC Porto.

Droo hiyo ya kufahamu timu zitakazomenyana kwenye hatua ya mtoano ya 16 bora itafanyika Jumatatu na hapo ndipo Mourinho atafahamu hatima yake katika kampeni za kuifanya Man United kufanya vizuri kwenye mchakamchaka wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.
 
TOTTENHAM Hotspur imekiri kuwa katika wakati mgumu kutokana na vita itakayokwenda kuikabili mwisho wa msimu katika kuhakikisha inambakiza kocha wake, Mauricio Pochettino.

Manchester United na Real Madrid ni miongoni mwa vigogo vinavyomsaka kocha huyo kwa ajili ya msimu ujao.
 
Jambo hilo limeripotiwa kuongeza presha kubwa huko kwenye kikosi cha Spurs kwa sababu kocha wake anawindwa na klabu kubwa na zenye pesa.

Pochettino mwenyewe alisema anataka kubaki Spurs kwa muda mrefu hadi mwakani itakaporudi kwenye uwanja wake mpya wenye thamani ya Pauni 1 Bilioni, lakini hakuonekana kupuuzia mpango huo wa kutakiwa Old Trafford na Bernabeu.
 
Kocha Jose Mourinho yupo kwenye hali mbaya huko Man United na huenda akafunguliwa mlango wa kutokea mwishoni mwa msimu huu kama hataiwezesha timu hiyo kumaliza ligi kwenye Top Four na kukosa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya yenye pesa kibao.
 
Real Madrid nayo inataka kumnasa kocha huyo baada ya sasa kuwa chini ya Santiago Solari baada ya kumfukuza kazi Julen Lopetegui baada ya miezi minne. Beki wa Spurs, Danny Rose alisema yeye kwa upande wake hashangazwi kabisa na kitendo cha Pochettino kuwindwa na klabu kutokana na mambo yake bora kabisa kwenye timu.
 
MWANASOKA bora wa dunia, fundi wa mpira Luka Modric ameripotiwa kugomea ofa ya mkataba mpya huko Real Madrid.

Kiungo huyo, ambaye hivi karibuni tu ametoka kushinda Tuzo ya Ballon d’Or alikuwa kwenye mipango ya Rais wa Real Madrid, Florentino Perez akimtaka aongeze mkataba wake kwenye kikosi hicho ili aendelee kubaki Santiago Bernabeu kwa muda mrefu zaidi.
 
Lakini, kinachoelezwa Modric amekataa ofa hiyo baada ya kuona mzigo uliowekwa mezani hauna hadhi yake.

Mchambuzi mahiri wa soka huko Hispania, Eduardo Inda alisema: “Rais alimpa ofa ya mkataba wa miaka miwili, lakini wenye thamanni ileile ya zamani, Euro 8 milioni kwa mwaka. Modric anataka mshahara upande na kuwa Euro 10 milioni, hivyo ya dili jipya limekwama. “Nina hofu kama Madrid itakubali kuongeza pesa mambo yanaweza kuwa mazuri.”

Mkataba wa sasa wa Modric huko Bernabeu utafika tamati 2020.
 
chupa ya coca
446529976_175802.jpeg
 
Back
Top Bottom