Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1fdhr9oescpwl.jpg
 
STAA wa Bayern Munich, James Rodriguez ameiambia familia yake kitu ambacho amepanga kwa sasa ni kurudi katika klabu yake ya zamani ya Real Madrid huko Bernabeu.

Kiungo huyo mshambuliaji, Rodriguez akiwa kwenye msimu wa pili wa miaka yake miwili ya mkopo huko Bayern, amesema mipango yake ni kurudi klabu hapo bila ya kujali kocha atakuwa nani kwa msimu ujao.
 
Kama ni (Santiago) Solari, (Jose) Mourinho, (Antonio) Conte au yeyote,” alisema James akiwaambia wanafamilia yake kuhusu mpango wake wa kurejea Santiago Bernabeu, baada ya kuona huko Bayern Munich mambo magumu chini ya Nico Kovac.

Rodriguez, ambaye ni Mcolombia kwa sasa yupo jijini Madrid akiuguza maumivu yake ya goti na ameamua kuweka mambo wazi kuwa, anataka kurudi kwenye chama lake la Los Blancos kitu ambacho kimeonekana kuungwa mkono na uongozi.
 
Bayern ina chaguo la kumbeba Rodriguez moja kwa moja kwa ada ya Euro 42 milioni, lakini mchezaji mwenyewe anachotaka kufanya ni kurudi Madrid mwakani.

Hata hivyo, jambo hilo litategemea na hali ya mambo huko Real Madrid kuhusiana na majaliwa ya wachezaji Isco, Gareth Bale na Karim Benzema, ambao kwa sasa ndio wako klabuni.
 
Back
Top Bottom