Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hakuna mtu mwenye tabu huku ulimwenguni kama mwafrika, lakini pamoja na tabu zote anazopitia maishani akifa hapumziki, anatakiwa tena awe mzimu wa kutatua matatizo ya ukoo wake.

Afrika tabu sana[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
tanzania_motorsports_47407458_151488625831302_7244863304136960059_n.jpg
 
Majina ya kukwepa kuitikia Msimu huu wa krismasi na Mwaka Mpya: Ukisikia mtu kakuita hivi, usiitike na usijaribu ku-smile hata kidogo, utakuja kinishukuru baadae!! 1. Mkubwa 2. Tajiri wangu 3. Boss wangu 4. Kiongozi 5. Mkurugenzi 6. Manager 7. Chief 8. Brigedia General 9. Honey 10. Dear nikuambie kitu..? 11.Mutu Ya Nguvuu 12.Mzee 13.Patroo 14. Kaka mukubwaaaaaa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Bro Kimbia tena kama hiyo 9 na 10 usigeuke hata nyuma!!

Hiyo namba 10 akiitamka wewe jifanye hujaisikia kabisaaa! [emoji1][emoji1][emoji1]
 
Kiungo mahiri wa Brazil, Philippe Coutinho, aliwashangaza wengi baada ya juzi kuwasili ghafla kwenye Uwanja wa ndege wa Liverpool akitokea nchini Hispania.

Mchezaji huyo mwenye miaka 26, aliihama Liverpool Januari mwaka huu na kujiunga na Barcelona ya Hispania kwa uhamisho wa Pauni 145 milioni ambapo tayari ameshaitumikia katika michezo 31 na kufunga mabao 12 akipika mengine manne.
 
Hata hivyo ilibainika baadaye kwamba alifunga safari hiyo ndefu ili kuitikia wito wa kuhudhuria sherehe ya siku ya kuzaliwa ya mke wa swahiba na Mbrazil mwenzake Roberto Firmino, Larissa Pereira.

Katika sherehe hizo Coutinho alijumuika na mastaa wengine kibao kutoka Brazil wakiwemo Alberto Moreno, Fabinho na wachezaji wengine kadhaa, pamoja na wachezaji wengine wa Liverpool.
 
Firmino alimwambia Coutinho kwa utani kuwa watu wote wanamtaka arejee Anfield, baadaye kidogo Moreno alirusha katika ukurasa wake wa Instagram akisema wamemmisi jambo lililosababisha mashabiki wengi kutuma ujumbe.

Wapo waliouliza sababu za ujio wake na wapo walimjtaka kubadili mawazo na kurejea Liverpool wakisema mchango wake bado unahitajika hasa ikizingatiwa kuwa umri wake bado mdogo.
 
Chelsea jana ilijihakikishia kutinga hatua ya 32 bora ya Europa Ligi ikiwa kinara wa kundi L, baada ya sare ya mabao 2-2 na MOL Vidi ya Hungary, lakini ikampoteza mshambuliaji wake Alvaro Morata.

Mshambuliaji huyo kutoka Hispania aliumia goti wakati akiunganisha krosi iliyopigwa na Callum Hudson-Odoi na kulazimika kutolewa uwanjani na nafasi yake kuchukuliwa na Olivier Giroud.
 
Kocha wa Chelsea, Maurizio Sarri, alisema kuumia kwa mshambuliaji huyo ni pigo kwani kwa sasa amebakiwa na mchezaji mmoja pekee wa nafasi hiyo aliye fiti Giroud.

Chelsea imekuwa timu ya kwanza kufunga mabao mwili yote kutokana na mipira ya adhabu ya moja kwa moja katika mechi moja ya Europa Ligi tangu Liverpool ilipofanya hivyo dhidi ya Zenit St Petersburg, Februari 2013.
 
Sare hiyo pia imeifanya Chelsea kuboresha rekodi yake ya kutopoteza mechi kufikia tisa mara ya mwisho ilifungwa na Ruben Kazan katika robo fainali ya msimu wa 2012-13.

Aidha Vidi nayo imekuwa timu ya kwanza kufunga mabao mawili dhidi ya Chelsea katika michuano hiyo tangu ilipofungwa na Ruben Kazan, Aprili 2013, timu hiyo imepoteza mechi mbili kati ya saba za michuano hiyo.
 
Back
Top Bottom