Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Fomula ya kukokotoa BMI ipo hata katika simu za Smart, kampuni za simu ziliona umuhimu kwa watumiaji kukotoa na kuanisha uzito wao wa mwili ili kujihadhari mapema na tatizo la unene.

Fomula hiyo huwa ni kukokotoa hesabu kwa kutafuta zao la mgawanyo wa uzito (kg) na urefu (m) kipeuo cha pili au urefu zidisha kwa urefu katika kipimo cha mita.
 
BMI inatumika kwa watu wenye umri wa miaka 18-65 ambayo kawaida ni kati ya 18.5-24.9, chini ya hapo au juu ya hapo ni tatizo kiafya. Ikiwa ni 25-30 ni uzito mkubwa na ikiwa 30 kuendelea ni uzito uliokithiri.

Fomula hii ndiyo inatuwezesha kuanisha zao la BMI, hivyo tunaweza kuanisha uzito wa mwili katika makundi kama vile uzito wa chini, uzito wa kawaida, uzito mkubwa, unene na unene uliokithiri.
 
Nasri atafanya hivi kushusha uzito uliokithiri

Hivi sasa Nasri ameanza mpango kamambe wa kushusha uzito kwa mazoezi mchanganyiko ya ‘gym’ na mepesi na huku akifuata programu maalum aliyopangiwa na mtaalam wa lishe za wanamichezo.

Ili kudhibiti wachezaji wasipate uzito uliokithiri ni jambo linalohitaji mpango maalumu kwa mtu binafsi, wataalamu wa afya ikiwamo madaktari, wataalamu wa lishe na wa mazoezi ya mwili.
 
Itamlazimu kula chakula ambacho kitawiana sawa mahitaji ya mwili na atahitajika kuwa na nidhamu ya hali ya juu ikiwamo kuepuka kula kiholela.

Maisha ya anasa, ulaji holela wa vyakula, kufungiwa kucheza soka na kutojihusisha na mazoezi kwa muda mrefu kulichangia Nasri kuongezeka uzito.
 
Uzito uliokithiri ni ishara ya mrundikano wa nishati ambayo ilingia mwili na haikutumika hivyo kubadilishwa na kuwa mafuta kwa ajili ya matumizi ya baadaye.

Mbinu za kudhibiti uzito huanzia kwenye mabadiliko ya kitabia kwa kufuata mwenendo na mtindo bora wa kimaisha, mazoezi, ratiba na aina ya mlo wa kula.
 
Itamlazimu kufanya mazoezi mepesi ya ziada ili mwili wake utumie mafuta yaliyorundikana na kushusha uzito, wakati huo huo atakuwa anakula vyakula vyenye kiasi kidogo cha nishati.

Vyakula hivyo ni kama vile nafaka isiyokobolewa, kupunguza kula vyakula vyenye sukari nyingi, vyakukaanga au vyenye mafuta mengi.
 
Mlo wake mkuu utakuwa ni nusu ya sahani ni mboga mboga na matunda, robo ikiwa nafaka isiyokobolewa na robo ni protini itokanayo na samaki na mimea jamii ya kunde.

Atahitajika kunywa maji mengi kuanzia lita 1.5-4 kwa siku pamoja na ulaji wa mboga mbichi na matunda mara kwa mara kama vyakula vya katikati kabla ya kula mlo mkuu.
 
Mazoezi atakayokuwa anafanya ni mazoezi mepesi ikiwamo kuogelea, kukimbia, kuruka kamba na kuchanganya na mazoezi ya magumu ya “gym” ikiwamo kubeba vyuma ili kujenga na kuimarisha misuli.

Uzito wake utakuwa unafuatiliwa kwa karibu na kunakiliwa kwa kuchorewa grafu ili kujua kama unapanda au unashuka.

Kupunguza uzito wa mwili sio kitu rahisi, Nasri atahitajika kushikamana na matibabu, maelekezo na ushauri toka kwa wataalam wa afya ili kufikia lengo la kupunguza kilo 11.
 
Endapo atafanikiwa kukabiliana na uzito huo kutamfanya kuwa mchezaji mtimilifu, mwepesi kimwili na kiakili hivyo kuweza kurudi upya na kunyumbulika kirahisi uwanjani.

Ukiacha wagonga nyundo klabu ya Everton nayo inamwinda kiungo huyo, tusubiri kuona hatma yake kama Nasri atafanikiwa kuzishusha kilo 11 na kusajiliwa klabu ya Westham.
 
1544894379496.png
msukuma wanaandamwa sana
 
Back
Top Bottom