Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Atakuwa ni mtu kutoka nje ya klabu hiyo, lakini hatakuwa meneja wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger.

Baadhi wanamzungumzia Zinedine Zidane aliyekuwa meneja wa Real Madrid.

Yupo pia meneja wa zamani wa Chelsea Mwitaliano Antonio Conte.

Yupo pia meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone na meneja wa sasa wa Tottenham Hotspur Mauricio Pochettino.
 
Jose Mourinho ametimuliw ana Manchester United baada ya kuwa na msimu mbaya katika klabu hiyo.
Taarifa ya klabu hiyo iliyochapishwa katika tovuti ilisomeka: 'Manchester United imetangaza kuwa Jose Mourinho imevunja mkataba na kocha huyo.
'Klabu ingependa kumshukuru Jose kwa kazi yake nzuri katika kipindi chote alichokuwa na Manchester United na tunamtakia maisha mema huko aendako.
 
Mreno huyo mwenye miaka 55, katika kikosi hicho cha Old Trafford amefanikiwa kutwaa mataji ya Kombe la Ligi na Europa Ligi katika miaka miwili na nusu aliyokaa.
Lakini kwa sasa Man United ipo nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa nyuma kwa pointi 19 baada ya kufungwa 3-1 na vinara Liverpool.
 
Kocha atakayechukua jukumu hilo kwa muda anategemea kutangazwa hivi karibuni, huku tukiendelea na utaratibu wa kusaka kocha mpya," ilisema taarifa ya Man United.

Manchester United ilinyanyaswa na kudhalilika dhidi ya Liverpool juzi Jumapili. Na sasa hali ni tete Old Trafford na mtu mmoja anaonekana amekalia kuti kavu na ndani ya timu hiyo maarufu. Jose Mourinho.
 
Katika pambano hilo Liverpool ilipiga mashuti 36 katika lango la United huku United ikifanya majaribio matano tu. Bao la tatu la Shaqiri lilikuwa linamaanisha United ilikuwa imefungwa mabao 29 katika mechi 17 wakati katika msimu mzima uliopita ilifungwa mabao 28 tu.
 
Manchester United ipo nyuma ya Liverpool kwa tofauti ya pointi 19 baada ya mechi 17 tu na haijawahi kutokea katika historia ya klabu hizo mbili. Ipo nyuma ya Chelsea inayoshika nafasi ya nne kwa pointi 11 na sasa wachambuzi wawili wanaoaminika katika soka la Kiingereza, Jamie Carragher na Gary Neville wanataka kocha huyo aondoke.
 
Baada ya kuitazama timu sio leo tu, bali msimu mzima, nimejiuliza, hii timu inaweza kweli kushinda ligi? Hapana. Hii ni timu ambayo inapaswa kuwa ya sita katika ligi? Hapana. Siamini kama kuna pengo kubwa la ubora kati ya Liverpool na United.
 
Nadhani Liverpool ilipambana zaidi. Hata hivyo, msimu huu siamini kama pengo inabidi liwe kubwa sana kama lilivyo sasa.

“Mourinho anapata ubora wa wachezaji wake? Hapana na wala hakaribii na huyu ni kocha wa kiwango cha juu. Mzunguko wake kama kocha mara zote unakuwa miaka miwili au mitatu. Anafanya makubwa miezi 18 ya kwanza baada ya hapo anachoka,” alisema Carragher.
 
Wakati Carragher akisema hayo, Neville anailaumu Bodi ya Manchester United kwa jinsi inavyoendesha mambo yake huku akiamini kocha huyo atafukuzwa msimu huu.

“Mourinho ataondoka? Nadhani itatokea, chaguo langu lilikuwa aende mpaka mwisho wa msimu. Hata hivyo, bodi haijiamini na inashangaza sana. Kumpa mkataba mpya wakati ikijua mwisho wa Mourinho katika makali yake unakuwa miaka mitatu. Mwaka wa tatu siku zote ni mgumu kwake,” alisema Neville.
 
Miezi 18 ya kwanza, United ilikuwa wa pili katika ligi ikitwaa mataji mawili katika msimu wake wa kwanza, hiyo ndiyo ingekuwa sababu ya bodi kuendelea kumfanya awe na njaa zaidi katika msimu wake wa tatu. Aliporudi tu katika maandalizi ya msimu mpya alichukiza na klabu ikashindwa kumudu hilo jambo.”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…