Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Alisema Pinto ni mtu mzuri mwenye majukumu ya kifamilia akiwa na mke na watoto watatu wanauthamini mchango wake na wataendelea kuwa karibu naye.

Nayo bodi inayosimamia Ligi Kuu Ureno imesema kwamba timu ya matibabu inaendelea kufanyia uchunguzi sampuli za maradhi aliyokuwa nayo ili kuangalia namna ya kufanikisha matibabu kwa kuwa bado haijasambaa mwilini.
 
Mchezaji wa kimataifa wa Colombia, Jeison Murillo, amesema kuwa anataka kudumu katika timu ya FC Barcelona aliyojiunga nayo kwa mkopo akitokea Valencia.

Mchezaji huyo ambaye tayari aliichezea Valencia mchezo mmoja wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, hataweza kuitumikia timu yake mpya ya Barcelona katika michuano hiyo kwa msimu huu.
 
Katika makubaliano ya klabu hizo mbili ni kwamba iwapo Barcelona itaamua kumsajili kwa mkataba wa kudumu beki huyo, italazimika kutoa Pauni 22.6 milioni.

Murillo mwenye miaka 26 aliyejiunga na Valencia baada ya kufanya vema wakati akicheza kwa mkopo kutoka Inter Milan ya Italia, alisema atahakikisha anapigania namba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…