Kocha wa timu ya Chongqing Dangdai Lifan ya Ligi Kuu ya China, Jordi Cruyff, ameionya Barcelona kujifunza kwa yaliyowakuta Real Madrid kwa Cristiano Ronaldo.
Cruyff kiungo wa zamani wa Barcelona na Manchester United, amesema anaamini kilichotokea kwa Real kitaikuta pia timu hiyo iwapo haitachukua tahadhari kuanzia hivi sasa.
Alisema Real licha ya kupokea ofa nyingi kwa Ronaldo, haikujiandaa kusaka warithi wake na sasa inateseka kwa pengo lakebaada ya kuhama ghafla Julai mwaka huu na pengo lake linaitesa. “Napenda kuwaambia viongozi wa Barcelona kilichowakuta Real kwa Ronaldo kitawakuta pia kwa Messi wasipochukua tahadhari,” alisema Cruyff.