Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Laporte apiga pasi hadi kero
Ligi Kuu England hadi ilipofika kwa sasa, beki wa kati wa Manchester City, Aymeric Laporte ndiye anayeongoza kwa kupiga pasi. Staa huyo wa huko Etihad, amepiga pasi 1,634. Hakuna mchezaji mwingine aliyepiga pasi nyingi hivyo kwenye ligi hiyo hadi kufikia Krismasi. Kiungo wa Chelsea, Jorginho anafuatia akiwa amepiga pasi 1,628 huku beki mwingine, Antonio Rudiger kutoka Chelsea akiwa kwenye nafasi ya tatu ya wapiga pasi nyingi hadi kero, akiwa amepiga 1,535 na kisha anafuatia kiungo Granit Xhaka wa Arsenal, ambaye amepiga pasi 1,498.
 
Hart shujaa wa kuokoa
Kipa wa Burnley, Joe Hart, ndiye aliyefunika kwa kuokoa hatari nyingi kwenye Ligi Kuu England hadi sasa, akiwa ameokoa mara 76. Hakuna kipa mwingine aliyeokoa hatari nyingi hivyo kama Hart, huku Neil Etheridge wa Cardiff akifuatia akiwa ameokoa hatari 71 na Lukasz Fabianski wa West Ham United akiwa ameokoa mara 69. Yule kipa matata kabisa anayesifika kwa sevu, David De Gea wa Manchester United, ameshika namba nne huko akiwa ameokoa mipira ya hatari mara 64.
 
Ubabe wa Top Six
Hadi kufikia kwenye mechi za Boxing Day, Man City ndio waliofunga mabao mengi zaidi 51, wakifuatiwa na Liverpool walifunga mara 43, kisha Spurs na mabao yao 42, Arsenal 41, Chelsea na Man United zikilingana kwa mabao 37 kila moja. Man City wameongoza pia kwa kupiga pasi, wakifanya hivyo mara 13,294, wakifuatiwa na Chelsea waliopiga pasi 13,146, Liverpool pasi 11,696, Arsenal pasi 10,800, Spurs wao wamepiga pasi 10,093 na Man United wakiwa wamepiga pasi 9,709. Man City wanaongoza pia kwa kupiga krosi, wakifanya hivyo mara 405 na kufuatiwa na Man United waliopiga krosi 366.
 
HUKO kitaa, mashabiki wa Liverpool wanapiga tu kelele kwamba wapewe tu taji lao la ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.
Wataachaje kutamba unadhani? Pointi 51 kileleni, hawajapoteza mechi yoyote na wamevuka Krismasi wakiwa wameweka pengo la pointi sita dhidi ya timu inayowafuatia kwenye msimamo huo.
 
Kocha wao, Jurgen Klopp anatamba na kusema kwamba wanataka kutengeneza historia ya kwao peke yao. Wakati Ligi Kuu England ikiwa imefika katikati, kwa maana ya kuchezwa mechi 19, Liverpool hawajui machungu ya kupoteza mchezo. Hii ni mara ya kwanza kwenye historia yao katika zama za Ligi Kuu, lakini ikiwa mara ya kwanza pia kwenye historia yao tangu walipokuwa moto miaka ya 1987 na 1988, ambapo walibeba ubingwa wakicheza mechi 29 bila ya kupoteza.
Liverpool hii imekuwa bora kuliko nyingine yoyote iliyowahi kutokea kwenye zama za Ligi Kuu England.
 
Wamecheza nusu msimu na hawajapoteza mechi yoyote. Lakini, kocha Klopp hataki kuwavimbisha vichwa wachezaji wake akiwaambia hilo hali halina maana yoyote, wapige mzigo. Klopp anasema anawaamini wachezaji wake mwamba wataendelea kutuliza akili zao ndani ya uwanja na kuangusha tu vichapo kwa wapinzani.
 
Tunataka kutengeneza historia yetu wenyewe kwa mara ya kwanza kwenye Ligi Kuu England, kwa mara ya kwanza hatujapoteza mechi kwa nusu msimu na kwamba tumeruhusu mabao saba tu," alisema Klopp.
"Namba zipo vizuri na hali pia ipo vizuri, lakini sitaki tujisahau, bado kuna mechi 19. Pointi sita hazina maana kubwa, hatujacheza na Arsenal na Man City. Vizuri tupo pointi sita juu ya timu nyingine, lakini itakuwa vyema kama tutaendelea kufanya kile ambacho tumekuwa tukitaka kukifanya siku zote, kuwa kwenye ubora hadi mwisho wa msimu kwa sababu sehemu ya kwanza ya msimu imeshakwisha.
 
Kocha Klopp anafurahia huduma bora kabisa kutoka kwa mastaa wake hasa kwa washambuliaji wake, wakiongozwa na Mohamed Salah, ambaye kwa sasa anatupia tu na kupambana kuwania Kiatu cha Dhahabu alichobeba kwenye ligi hiyo msimu uliopita. Hadi sasa Mo Salah amefunga mabao 12, moja nyuma ya kinara fowadi wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang.
 
Kwenye mechi iliyopita, Liverpool waliichapa Newcastle United na kusema alishangazwa na kusikia kelele kubwa kutoka jukwaani kumbe hiyo ilitokana na kupata taarifa kwamba Man City kachapwa na Leicester City.
Dada nikufanyie mchongo uwe mtangazaji kipindi cha michezo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini Merson alisema kuwa kusema timu imepanda kiwango ni uongo na aibu kwa wachezaji wa timu hiyo.

Mabadiliko ya Man United si kwa sababu ya Ole Gunnar Solskjaer. Suala hapa ni wachezaji na ni kama wanaleta utani,’ alisema mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal na England akizungumza na Sky Sports.
 
Ukiwaangalia, tofauti inayoonekana ni kama utani tu, wachezaji walichukiza sana. ‘Naona aibu. Hivi kweli mara tu Solskjaer anaonekana bonge la kocha kwa asilimia 100 kuliko Jose Mourinho?

“Come on…. sijaipenda kabisa hii. Nimeshangaa wachezaji wote wanakimbia uwanjani, na tunatarajia kuona ushindi mwingine wa mabao 4-0.
 
Wachezaji ni watu wazima, wanatakiwa kusema ukweli kama alivyofanya Valencia kama walichokuwa wanakifanya uwanjani. Lakini uwamuzi ni wao wachezaji wenyewe…’

Ushindi wa Cardiff umeifanya timu hiyo kubakia nafasi yake ya sita ikiwa nyum kwa pointi nane za Chelsea.
 
Back
Top Bottom