Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wwe
FB_IMG_1546161052287.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
#TANGAZO MAALUM

Nyie Watu Wa Mjini... Hii Tabia Ya Kuja Kijijini Kwa Ajili Ya Sikukuu Mnakuja Na Sukari Kilo 02, Unga Wa Ngano Kilo 03, Pilipili Kopo 03, Sabuni Miche 02, Tomato Sauce Kopo 04 Kisha Mnakaa Kijijini Siku 02 Mnaaga Kurudi Mjini... Halafu Mnataka Tuwape Mahindi Debe 06, Mchele Kilo 40, Kuku 05 Na Mihogo Debe 08.. Mjue Tumepiga Hesabu, Kikokotoo Mlichotumia Kinatuibia 105%.. [emoji23][emoji16][emoji3][emoji1][emoji7][emoji39][emoji38][emoji16][emoji26]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KRISMASI imepita na Liverpool wameketi kwenye kilele cha msimamo wa Ligi Kuu England.
Pointi 51 kibindoni zinatosha kwa kikosi hicho cha Jurgen Klopp chenye maskani yake Anfield kuamsha matumaini ya kubeba ubingwa wao wa kwanza wa Ligi Kuu England msimu huu.
 
Shughuli ipo kwa Pep Guardiola huko Etihad, chama lake la Manchester City limechapwa kwenye mechi mbili mfululizo na sasa kuporomoka hadi kwenye nafasi ya tatu katika msimamo huo, wakiwa na pointi 44, saba nyuma ya vinara Liverpool.
Tottenham Hotspur wapo kwenye nafasi ya pili na pointi 45, huku Chelsea wakikamilisha Top Four na pointi zao 40, huku Arsenal wakiwa kwenye nafasi ya tano na pointi 38 na Manchester United, chini ya kocha wao mpya Ole Gunnar Solskjaer wapo kwenye nafasi ya sita na pointi zao 32. Man United imeachwa nyuma kwa pointi 19 na vinara wa ligi hiyo hadi kufika sasa.
 
Kila mtu ana kiboko yake, lakini unafahamu ni nani kwenye Ligi Kuu England hadi ilipofikia kwa sasa ikiwa imechezwa mechi za Boxing Day?

Aubameyang afunga kuliko wote
Kwenye Ligi Kuu England hadi kufikia Krismasi, straika wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang ndiye mchezaji aliyefunga mabao mengi kuliko mchezaji yeyote kwenye ligi hiyo. Staa huyo hadi sasa amefunga mabao 13 na kufuatiwa na mastaa wawili, Harry Kane wa Tottenham na Mohamed Salah wa Liverpool ambao kila mmoja amefunga mabao 12 na hivyo kufanya mchakamchaka wa kuwania Kiatu cha Dhahabu kwenye ligi ya msimu huu kuwa na mvuto mkubwa.
 
Hazard aongoza kwa asisti
Supastaa wa Chelsea, Eden Hazard amefunga mabao 10 kwenye Ligi Kuu England hadi kufikia Krismasi na kwamba na yumo kwenye mbio za kuwania tuzo ya ufungaji bora. Lakini, staa huyo amekuwa moto zaidi kwenye kuasisti, akipiga pasi zilizozaa mabao mara nyingi kuliko yeyote kwenye ligi hiyo hadi sasa. Hazard amepiga asisti tisa na kufuatiwa na Ryan Fraser wa Bournemouth, aliyepiga asisti nane, huku Christian Erikssen wa Tottenham na Leroy Sane, wamefuatia na asisti zao saba kwa kila mmoja.
 
Back
Top Bottom