Ubabe wa Top Six
Hadi kufikia kwenye mechi za Boxing Day, Man City ndio waliofunga mabao mengi zaidi 51, wakifuatiwa na Liverpool walifunga mara 43, kisha Spurs na mabao yao 42, Arsenal 41, Chelsea na Man United zikilingana kwa mabao 37 kila moja. Man City wameongoza pia kwa kupiga pasi, wakifanya hivyo mara 13,294, wakifuatiwa na Chelsea waliopiga pasi 13,146, Liverpool pasi 11,696, Arsenal pasi 10,800, Spurs wao wamepiga pasi 10,093 na Man United wakiwa wamepiga pasi 9,709. Man City wanaongoza pia kwa kupiga krosi, wakifanya hivyo mara 405 na kufuatiwa na Man United waliopiga krosi 366.