Hadi Ijumaa, Ozil alifanya mazoezi na wenzake kwa ajili ya kujiunga na kuwakabili Liverpool, lakini baadaye ikafichuka kwamba jina lake limeondolewa kwa kikosi kwa sababu anaumwa goti. Sawa, majeruhi yamekuwa yakitokea na wachezaji wamekuwa wakikosa mechi kila wiki, lakini hili linaloendelea huko Arsenal, Ozil ana bahati mbaya. Mashabiki hawaelewi kwanini majeruhi ya Ozil yamekuwa yakitokea kwenye mechi kubwa tu. Enzi za Arsene Wenger, sawa Ozil alikuwa akikosa baadhi ya mechi, lakini hilo lisingefanyika kwenye mechi dhidi ya Liverpool.