Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

The%20GOAT%20Vs%20Wapigania%20matumbo%20uchwara.gif
 
Hapo sasa.

Pengine kwa vile mwanaume ndiye mwenye maamuzi katika hili suala...

Ila jamaa naye hana huruma. Miaka 11 mingi sana aisee....
Kwel bro,,miaka 11 ni mingi sana,

Ila kwenye masuala ya mahusiano ni ngumu sana kujua mwenyew tatzo,,maana kila mmoja wao hapa atakuja na sababu zake

Hapa tumepata maelezo ya upande mmoja tu,,usikute jamaa na yy anasababu zake zlzopelekea kukaa juu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MWAKA 2018 umehusisha matukio kibao kwenye soka hasa linapokuja usajili. Kwenye suala hilo la usajili kuna dili kadhaa zilifanywa ambazo zilivunja rekodi kwa mwaka huu na kusubiriwa kama zitaweza kuvunjwa kwenye usajili utakaofanyika mwakani.

Ikiwa ni jambo la kawaida tu kwenye soka la kisasa timu kutumia pesa nyingi kwenye kusajili nyota wapya, hii hapa ndio orodha ya usajili uliovunja rekodi huko Ulaya mwaka huu wa 2018.
 
5.Virgil van Dijk (Beki ghali duniani)

Licha ya kwamba dili hilo lilimalizwa kwenye wiki ya mwisho ya mwaka 2017, beki wa kati Virgil van Dijk alijiunga rasmi na Liverpool kwenye dirisha la Januari mwaka huu akitokea Southampton. Kwenye uhamisho huo, Liverpool walilipa kiasi cha Pauni 75 milioni kupata huduma ya Mdachi huyo na hivyo jambo hilo kumfanya Van Dijk kuwa beki ghali zaidi duniani. Hata hivyo, hayakuwa matumizi mabaya ya pesa kwani tangu beki huyo alipotua Anfield amekwenda kumaliza kabisa tatizo lililokuwa likimuumiza kichwa kocha, Jurgen Klopp la kuwa na safu ya mabeki wanaopitisha tu mabao. Van Dijk amekuwa akifanya vizuri kwenye beki huko akitumiza mambo mengine ikiwamo ya kufunga mabao ili kuipa ushindi timu yake ambayo ndio vinara wa Ligi Kuu England msimu huu.
 
4.Alisson Becker (Kipa ghali duniani)

Wakiwa wamemsajili, Mohamed Salah kutoka AS Roma kwenye majira ya kiangazi mwaka jana, Liverpool kwenye majira kama hayo ya mwaka huu waliamua kurudi tena kwenye timu hiyo kwenda kutafuta suluhu ya tatizo lao lililokuwa likiwakabili kwenye goli lao. Liverpool walikwenda kumsajili kipa wa Kibrazili, Alisson Becker. Hata hivyo, AS Roma hawakuwa tayari kumwaachia kipa huyo kwa bei ya kitoto na hivyo kuwalazimisha wababe hao wa Anfield kulipa Pauni 66.9 milioni kupata huduma ya kipa huyo. Kupatikana kwa kipa huyo kunaonekana kuwa ni usajili bora kabisa uliowahi kufanywa na kocha, Jurgen Klopp kwenye kikosi hicho cha Liverpool kwani hadi kufikia kwenye mechi ya jana Jumatano kwenye Ligi Kuu England walikuwa wenyewe tu ambao hawakupoteza mechi yoyote msimu huu. Alisson aliweka rekodi ya kuwa kipa ghali duniani, lakini baadaye rekodi yake ilikuja kuvunjwa na Kepa siku chache baadaye.
 
3.Kepa Arrizabalaga (Kipa ghali, ampiku Alisson)

Kepa Arrizabalaga amevunja rekodi iliyokuwa imewekwa siku chache na Mbrazili, Alisson Becker ya kuwa kipa ghali duniani. Chelsea ndio waliovunja rekodi huyo wakati walipoamua kumnunua Kepa kwa ada ya Pauni 71.6 milioni kwenda kuziba pengo la Mbelgiji, Thibaut Courtois, aliyeamua kulazimisha uhamisho wa kwenda kujiunga na Real Madrid. Kepa alikuwa kipa wa Athletic Bilbao na kiwango hicho cha pesa kilicholipwa na Chelsea ndicho kilichokuwa kimeandikwa kwenye mkataba wake kwamba kama kuna timu inamtaka basi itapaswa kulipia ili kuuvunja. Kepa amekuwa mhimili mzuri kwenye goli la wababe hao wa Stamford Bridge na jambo hilo linaonyesha kwamba pesa iliyotumika kunasa huduma yake ilitumika vyema, haikununua mfanyakazi hewa.
 
2.Philippe Coutinho (mchezaji ghali La Liga)

Philippe Coutinho alihamia Barcelona akitokea Liverpool kwa ada ya Pauni 105 milioni, ambayo itaongezeka na kufikia Pauni 142 milioni kutokana na kiwango chake atakachokionyesha ndani ya uwanja. Kutokana na hilo kwa uhamisho huo uliofanyika kwenye dirisha la Januari mwaka huu, staa huyo wa Kibrazili anakuwa mchezaji aliyenaswa kwa pesa nyingi, akiwa mchezaji ghali kwa mwaka huu huko kwenye La Liga. Jambo hilo limemfanya apiku utawala wa Ousmane Dembele, ambaye alikuwa akishikilia rekodi hiyo ya kuwa mchezaji aliyesajiliwa kwa pesa nyingi kwenye La Liga kwenye majira ya kiangazi mwaka 2017. Mbrazili Coutinho ameanza vizuri kwenye kikosi cha Barcelona licha ya kwamba bado hajatunza ubora wake kwa muda mrefu kwenye kikosi hicho cha Nou Camp.
 
Back
Top Bottom