4.Alisson Becker (Kipa ghali duniani)
Wakiwa wamemsajili, Mohamed Salah kutoka AS Roma kwenye majira ya kiangazi mwaka jana, Liverpool kwenye majira kama hayo ya mwaka huu waliamua kurudi tena kwenye timu hiyo kwenda kutafuta suluhu ya tatizo lao lililokuwa likiwakabili kwenye goli lao. Liverpool walikwenda kumsajili kipa wa Kibrazili, Alisson Becker. Hata hivyo, AS Roma hawakuwa tayari kumwaachia kipa huyo kwa bei ya kitoto na hivyo kuwalazimisha wababe hao wa Anfield kulipa Pauni 66.9 milioni kupata huduma ya kipa huyo. Kupatikana kwa kipa huyo kunaonekana kuwa ni usajili bora kabisa uliowahi kufanywa na kocha, Jurgen Klopp kwenye kikosi hicho cha Liverpool kwani hadi kufikia kwenye mechi ya jana Jumatano kwenye Ligi Kuu England walikuwa wenyewe tu ambao hawakupoteza mechi yoyote msimu huu. Alisson aliweka rekodi ya kuwa kipa ghali duniani, lakini baadaye rekodi yake ilikuja kuvunjwa na Kepa siku chache baadaye.