1.Cristiano Ronaldo (mchezaji ghali Serie A)
Cristiano Ronaldo aliwaduwaza wengi kwa uamuzi wake wa kwenda kujiunga na Juventus baada ya kuachana na Real Madrid kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya. Mabingwa hao wa Italia walilipa zaidi ya Euro 100 milioni kunasa huduma ya Mreno huyo huku kukiwa na makubaliano ya kulipa Euro 12 milioni nyingine baadaye kutokana na kiwango chake cha ndani ya uwanja. Jambo hilo linamfanya Ronaldo kuwa mchezaji ghali zaidi huko kwenye ligi ya Serie A. Maisha yake ndani ya kikosi cha Juventus yanaonekana kuwa sawa ambapo hadi sasa ameshafunga mabao 12 na kuasisti saba katika mechi 22 alizocheza.