BAADA ya Liverpool kupokea kichapo cha 2-1, kutoka kwa Manchester City, kiungo wa Man City, Leroy Sane amesema
Fernandinho ndiye alikuwa mchango mkubwa katika ushindi huo.
Akizungumza na mtandano wa Tribal Football baada ya mchezo kumalizika, Sane alisema kwamba kila mmoja anajua kabisa kwamba Fernandinho ni mchezaji muhimu katika kikosi chao siku zote kwa hiyo uwepo wake umefanya waibuke na ushindi katika mchezo huo.