Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Msimu ujao wanaweza kuibuka watu wengine wenye kasi. Arsenal wanazidi kujenga timu. Manchester United inajitafakari. Tottenham na Chelsea zinajipanga upya. Manchester City wameonekana kuanza kuwa na miguu mizito lakini watarudi vema zaidi.
 
Baada ya miaka mingi ya kuishia karibu, huu ni msimu ambao Liverpool inabidi wamalize mbio. Na uzuri wa saikolojia ya mpira ni kwamba kama Liverpool wakichukua ubingwa msimu huu basi wataweza kuchukua tena na tena katika miaka hii inayokuja. Kila mtu atajiamini klabuni. Kwa sasa mzimu unawaandama na baada ya mechi ya juzi Etihad unaweza kukuta bahati mbaya zinaanza kuwa nyingi.
 
Kila la kheri Anfield. Miaka 28 ni mingi kwa timu ambayo bado ni kubwa kutochukua ubingwa wa Ligi. Timu ambayo bado ina pesa, timu ambayo bado ina utamaduni mkubwa, timu ambayo ni Liverpool na imeendelea kuishi Kiliverpool. Tatizo ni nini hasa? Nadhani safari hii wanaweza kuondoa nuksi. Kama tu wataendelea kushikilia kamba.
 
Hawa wa leo wanaweza kuweka historia kama wakishikilia kamba vema. Mechi 17 zilizobaki zinaonekana kuwa chache huku wakiwa wanaongoza kwa tofauti ya pointi sita. Lakini wenye kumbukumbu zetu tunafahamu kwamba Liverpool waliwahi kuwepo mahala pazuri zaidi ya hapo. Tatizo lilikuwa lile lile la pumzi za kushikilia kamba mpaka dakika ya mwisho.
 
Kula hiyo
FB_IMG_1546618643033.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom