Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Si unajua hadi kufikia asubuhi ya juzi Alhamisi, Liverpool walikuwa wakiongoza ligi kwa tofauti ya pointi saba. Ndio, pointi saba. Lakini, shida ni kwamba usiku wake walikuwa na mechi dhidi ya Manchester City uwanjani Etihad. Kocha, Jurgen Klopp alipanga kwenda kushinda mechi hiyo ili kuweka pengo la pointi 10, ambako hakika lingemfanya kuwa na uhakika walau wa asilimia 70 kubeba ubingwa wa ligi hiyo kwa msimu huu.
Lakini, hilo halikuwa kwenye akili ya Pep Guardiola. Aliingiza uwanjani kikosi chake cha Man City na mbinu kibao za kiufundi. Hivyo, hivi unavyosoma hapa, pengo limebaki pointi nne tu, kufanya mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England kuanza upya
 
Hakuna mwenye uhakika. Hata, Tottenham Hotspur wataanza kupiga hesabu za kubeba ubingwa huo.
Utashangaa hata Manchester United, Chelsea, Arsenal nao watakuwa na matumaini ya kubeba taji hilo baada ya kile kilichofanywa na Leroy Sane hiyo juzi huko Etihad.
 
Msimamo unavyosomeka ni kwamba Spurs wao wapo pointi sita kuwafikia Liverpool kileleni. Lakini, matumaini yanakwenda pia kwa Man United kwa sababu kabla ya mechi hiyo kupigwa, pengo la pointi lilikuwa 19, lakini zimepungua na kufikia 16. Wanaamini chochote kinaweza kutokea kwa sababu bado kuna mechi kibao tu za kuchuana wenyewe kwa wenyewe kama ilivyokuwa kwa usiku huo wa juzi.
 
Ilikuwa fainali kwetu kwa sababu tungefungwa basi mambo yangekuwa yamekwisha hapohapo. Lakini, kwa sasa dude limerudi upya, tunapumua,” alisema Guardiola.
Ligi hiyo hadi sasa zimeshachezwa mechi 21, hivyo kuna mechi 17 za kucheza, sawa na pointi 51 jambo linalofanya moto wa mchakamchaka wa kuwania ubingwa kuwa ndio kwanza unaanza.
 
OLE Gunnar Solskjaer amepania kufanya mambo makubwa kwenye kikosi cha Manchester United ili kukamatia dili la kudumu. Katika kuwaweka sawa mastaa wake, amepanga kwenda kuweka kambi ya mazoezi huko Dubai kuanzia wiki ijayo.
 
Jumamosi watakipiga na Reading kwenye Kombe la FA na baada ya hapo, watakwea pipa kwenye huko Mashariki ya Kati watakakokaa kambi ya siku nne katika hoteli moja matata kabisa ya nyota tano, One&Only Royal Mirage Arabian Court Hotel.
 
Hoteli hiyo ya kisasa kabisa watakayofikia Man United, usiku mmoja kulala ni Pauni 350, lakini Solskjaer hafanyi mtoko huo kwa ajili ya kwenda kula bata, bali kwenda kutafuta hali ya joto ili kujiweka sawa kabla ya kurudi kwenye mchakamchaka zaidi wa Ligi Kuu England.
 
Solskjaer, ambaye ameiongoza Man United katika mechi nne na kushinda zote huku kikosi chake kikifunga mabao 14, dhamira yake ni kuifanya timu hiyo kuwa moto hasa katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu England. Kibarua chake kwa sasa kinahesabika kama cha muda hadi mwisho wa msimu baada ya kuchukua mikoba ya kuinoa timu hiyo kutoka kwa Jose Mourinho, aliyefutwa kazi mwezi uliopita.
 
Ole anaamini mtoko huo utawafanya wachezaji wake kurudisha umoja zaidi, lakini pia akipanga kwenye kuwafanya kuwa fiti huku akitarajia kuwajaza mbinu zake zaidi ili watakaporudi England wawe na akili moja tu, kufanya kweli kwenye Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 
Solskjaer amerudisha morali kwenye kikosi hicho tangu alipochukua jukumu la kuinoa mwezi uliopita, wakati huo nyuma hali ilikuwa mbaya kwelikweli. Paul Pogba na Luke Shaw ni moja ya wachezaji walionekana kupanda viwango vyao chini ya kocha huyu, huku wachezaji kama, Ander Herrera na Anthony Martial wakianza kutumika vyema kwenye kikosi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…