Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Solskjaer amerudisha morali kwenye kikosi hicho tangu alipochukua jukumu la kuinoa mwezi uliopita, wakati huo nyuma hali ilikuwa mbaya kwelikweli. Paul Pogba na Luke Shaw ni moja ya wachezaji walionekana kupanda viwango vyao chini ya kocha huyu, huku wachezaji kama, Ander Herrera na Anthony Martial wakianza kutumika vyema kwenye kikosi.
 
Solskjaer ameonyesha upande wake wa ukali pia, ambapo alimbwatukia Martial baada ya kuchelewa mazoezini siku ya Krismasi, jambo lililomfanya winga huyo Mfaransa kufuta akaunti zake zote za mitandao ya kijamii.
 
Solskjaer alisema: "Kamwe usijisahau mahali ulipo na nembo unayovaa unapokuwa uwanjani kwa sababu sisi ni klabu yenye historia kubwa tofauti na wengine. Tuna utamaduni tofauti. Tulikuwa na bosi bora kabisa duniani, tulikuwa na Sir Matt kabla ya hapo. Tunataratibu zetu na tuna mfumo wetu wa kiuchezaji."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…