Timu hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa kwenye safu ya ushambuliaji kwani Mkorea, Son Heung-Min hivi karibuni atakwenda kujiunga na timu yake ya taifa kwa ajili ha mashindano ya Asia hivyo iwapo Kane akiumia watabaki na mshambuliaji mmoja tu wa kati ambaye ni Fernando Llorente.
Tottenham inakabiliwa na ratiba ngumu katika kipindi cha hivi karibuni jambo ambalo linawalazimisha kucheza kwa tahadhali kubwa ili isiweze kuwaathiri.
Tottenham inakabiliwa na ratiba ngumu katika kipindi cha hivi karibuni jambo ambalo linawalazimisha kucheza kwa tahadhali kubwa ili isiweze kuwaathiri.
Kwa sababu tofauti niliamua kufanya mabadiliko na kumuingiza Kane lakini kubwa kuliko zote ilikuwa ni muhimu kuonyesha heshima kwa watu wa hapa ili wamuone Harry Kane ambaye ni staa wa soka la England’, alisema Pochettino
Kocha wa muda wa Manchester United, Ole Gunnar Solskajer anaamini yeye ni mtu sahihi wa kuiongoza klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi ya jinsi alivyo sasa.
Tangu alipoteuliwa kuinoa kwa muda Manchester United, Solskjaer ameiongoza kuibuka na ushindi kwenye mechi nne mfululizo tena ikicheza soka safi na kufunga mabao mengi kwenye michezo yake.
Matokeo hayo ya ushindi wa mechi nne mfululizo yameonekana kumpa nguvu Solskjaer ya kuomba aendelee kudumu kwenye nafasi hiyo kwa muda mrefu badala ya kuajiri kocha mwingine.
Manchester United inaniendana na mimi kwa sababu ipo ndani mwangu. Ni milango ya mapema. Wakati nakuja, walikuwa wawazi na waaminifu wakaniambia kwamba wanatafuta kocha mpya lakini kadri unavyokaa hapa ndivyo unapovutiwa zaidi,” alisema Solskjaer.