Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Beki wa Ajax anayechezea timu ya taifa ya Uholanzi Matthijs de Ligt, 19, amehimizwa kukataa kuhamia Juventus na badala yake ajiunge na Manchester United. (Manchester Evening News)
 
Real Madrid wameanza harakati za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Denmark Christian Eriksen, 26, kutoka Tottenham na wanajiandaa kutoa takriban £100m kumnasa. (Independent)
 
Juventus wanasema wanaweza wakashawishika kumuuza Paulo Dybala, 25, ambaye anatafutwa na Manchester City mwisho wa msimu, lakini mradi tu ada ya uhamisho wa raia huyo wa Argentina iwe zaidi ya £90m. (Tuttosport kupitia Express)
 
Borussia Dortmund na Bayern Munich wanatarajiwa kuwasilisha ofa kumtaka mshambuliaji wa RB Leipzig anayechezea timu ya taifa ya Ujerumani Timo Werner, 22, ambaye pia amehusishwa na kuhamia Liverpool. (Bild)
 
Chelsea wanamnyatia kiungo wa kati wa Cagliari Nicolo Barella ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa £45m, lakini huenda wakakumbana na ushindani kutoka kwa Napoli na Inter Milan ambao pia wanataka saini ya kijana huyo wa miaka 21. Mchezaji huyo hata hivyo anadaiwa kutotaka kuihama klabu hiyo ya Serie A wakati wa dirisha la sasa la uhamisho wa wachezaji. (Goal.com)
 
Unai Emery amewahimiza Arsenal kutafuta pesa za kukamilisha ununuzi wa kiungo wa kati wa Barcelona Denis Suarez, 25, mwezi huu. Klabu hiyo ya Uhispania inadaiwa kuwa tayari kumwachilia mchezaji huyo kwa mkopo iwapo kutakuwa na ahadi ya kutoa £20m kumchukua Suarez kwa mkataba wa kudumu mwisho wa msimu. (London Evening Standard)
 
Unai Emery amewahimiza Arsenal kutafuta pesa za kukamilisha ununuzi wa kiungo wa kati wa Barcelona Denis Suarez, 25, mwezi huu. Klabu hiyo ya Uhispania inadaiwa kuwa tayari kumwachilia mchezaji huyo kwa mkopo iwapo kutakuwa na ahadi ya kutoa £20m kumchukua Suarez kwa mkataba wa kudumu mwisho wa msimu. (London Evening Standard)
 
Arsenal wapo katika nafasi nzuri ya kumnunua mshambuliaji wa Ubelgiji Yannick Carrasco. Mchezaji huyo wa miaka 25 aliihama Atletico Madrid na kujiunga na klabu ya Dalian Yifang inayocheza Ligi Kuu ya Uchina Februari mwaka jana. (Mirror)
 
West Ham wanamnyatia mshambuliaji wa Inter Milan kutoka Brazil Gabriel Barbosa. Mchezaji huyo wa miaka 22 - ambaye alikaa klabu ya Santos ya Brazil kwa mkopo miezi 12 iliyopita - amependekezwa kwa West Ham kwa mkpo hadi mwisho wa msimu. (Mirror)
 
Meneja wa Southampton Ralph Hasenhuttl amethibitisha kwamba klabu hiyo imepokea ofa kutoka kwa klabu zinazomtaka mshambuliaji wa Italia Manolo Gabbiadini, 27. (Daily Echo)
 
Meneja wa Derby Frank Lampard hajafanikiwa katika juhudi zake za kutaka kumchukua kiungo wa kati mkabaji Ethan Ampadu, 18, kutoka kwa klabu yake ya zamani Chelsea. (Independent)
 
AC Milan wanamtafuta mshambuliaji wa Genoa na Poland Krzysztof Piatek, 23, wakitaka kumtumia kujaza pengo litakaloachwa na mshambuliaji wa Argentina Gonzalo Higuan, 31. (La Gazzetta dello Sport)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…