Van Gaal alisema Man City inamiliki wachezaji wawili, lakini Klopp ameonyesha kuwa ni kocha bora kuliko Guardiola.
Mdachi huyo ana uzoefu mkubwa katika kubeba mataji ya ligi, akifanya hivyo mara saba huko Uholanzi, Hispania na Ujerumani na aliwahi kuinoa Man United, ambapo aliishia kushika nafasi ya nne na tano kwenye msimamo katika misimu yake miwili aliyodumu Old Trafford.