Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

received_339164946933544.jpeg
 
FAHAMU || Mwanamuziki wa Kongo Kofii Olomide ana shahada ya uzamili katika hesabu (Master's Degree in Mathematics), yaani ni mtaalamu wa mahesabu ingawa tangu ahitimu mwaka 1980 hajawahi kuifanyia kazi.
 
Mbali na kipaji cha kusakata soka, lakini juhudi, uvumilivu na kujituma ni miongoni mwa vitu vinavyoweza kumbeba mchezaji kupata mafanikio.

Bila shaka unakumbuka jina la beki wa kushoto wa zamani wa timu ya vijana ya Chelsea, Adam Nditi mwenye asili ya Tanzania. Hakuna aliyefikiri anaweza kupotea kwenye ramani ya soka.
 
Nditi alizaliwa kwenye familia ya mpira kutokana na baba yake mzee Erick Nditi kucheza soka kipindi chake cha ujana akiwa na klabu ya Kikwajuni na timu ya Taifa ya Zanzibar. Mzee huyo aliondoka Tanzania mwaka 1995, inatajwa alizamia Uingereza baada ya kukutana na mrembo wa Kiingereza Marina ambaye ana asili ya Italia na Uingereza. Alifikia katika Kitongoji cha Basingstoke.
 
Wakati huo tayari alikuwa ameacha mtoto Zanzibar ambaye ni Adam aliyezaa na mwanamke mmoja wa Tanzania mwaka 1994 wakati akikaribia kuacha soka katika klabu ya Kikwajuni.
 
Wakati huo tayari alikuwa ameacha mtoto Zanzibar ambaye ni Adam aliyezaa na mwanamke mmoja wa Tanzania mwaka 1994 wakati akikaribia kuacha soka katika klabu ya Kikwajuni.
 
Nditi alimfuata baba yake Uingereza na baada ya kuwasili nchini humo alijihusisha na soka na baadaye alipata nafasi ya kujiunga na akademi ya Chelsea.

Kinda huyo alijiunga na akademi hiyo mwaka 2006 akicheza timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 18 ambako alikutana na akina Charly Musonda Jr, Andreas Christensen na Reuben Loftus-Cheek.
 
Umri ulivyosogea alipandishwa hadi kikosi cha vijana wenye umri chini ya miaka 21 cha Chelsea ambacho kinashiriki ligi kwa vijana wenye umri huo.

Akiwa na kikosi cha Chelsea alipata nafasi ya kucheza mara kwa mara na moja ya mchezo ambao alicheza ni ule wa nusu fainali ya Kombe la FA, Aprili 10, 2011 kati ya timu yake iliyokuwa ikichuana na Manchester United.
 
Man United kilikuwa na Paul Pogba ambaye kwa sasa ni tegemeo la kikosi hicho. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa amewahi kutamba na Juventus kabla ya kurejea Old Trafford. Maisha yaliendelea kwa Nditi na mwishowe akaingia katika kikosi cha kwanza cha Chelsea akipewa jezi namba 47, lakini kwa bahati mbaya ndiyo ukawa mwanzo wa kupotea.
 
Kinda huyo alijikuta akitemwa baada ya kutoonyesha kiwango bora kwenye mazoezi ya kikosi hicho cha matajiri wa London na alipoondoka Chelsea alikaa muda mrefu bila ya kupata timu ndipo alipoibukia Fleetwood, iliyokuwa daraja la pili (League One).
 
Back
Top Bottom