Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

455024338_103290.jpeg
 
Leo kwa pamoja twende tukakumbushane ni namna gani ya kuishi maisha yako, wengi wetu hivi sasa tumejikuta tumetoka kabisa nje ya mstari tumejikuta tunaishi maisha yasiyoyetu kabisa, yawezekana ni yamrafiki zetu, wapenzi wetu, jamaa zetu , watu wetu wakaribu na wengine wamefika mbali na kujikuta wanaishi maisha ya watu wanaowaona kwenye mitandao, wamesahau kuwa na wao wanamaisha yao yofauti na yale ya wengine wanayotamani kuyaishi kila siku bila mafanikio yoyote,
 
Eti kwa sababu umemuona rafiki yako anaishi maisha ya starehe basi na wewe unataka uishi hivyo hivyo wakati sio maisha yako na hayawezi kuwa yako, hamuwezi kuishi maisha sawa wakati kila mtu anamalengo yake na ndoto zake, wewe kama malengo yako ni kuwa tajiti mkubwa miaka kumi ijayo hauwezi ukaishi maisha sawa na mtu ambaye malengo yake ni kuwa mwalimu miaka mitatu ijayo, nyie ni watu wawili tofauti kimawazo kimtazamo na hata kimaisha kwa ujumla,
 
Ndoto yako yaweza kuwa ukipata pesa ujenge nyuma na ndio maisha yako, ukipata hiyo pesa sasa unajikuta unasahau ndoto au malengo yako unaanza kutimiza ndoto za mwingine eti kwa sababu umemuona jamaa yako kanunua gari basi unaghaili kujenda nyumba unaenda kununua gari, hapo unakuwa umehama maisha yako na kwenda kuishi maisha ya mwingine, Au mwingine umezoea kuvaa nguo za heshima mara ukamuona mtu kwenye mtandao kavaa nguo zisizo na maadili eti kwasababu tu ni shabiki wake au mnafanana umbo basi na wewe utataka kuvaa mavazi kama yake, huko ni kukengeuka ni kuishi maisha ya wengine ambayo hayatakufikisha popote zaidi ya kukupotezea mda tu, maana hata uige maisha ya wengine vipi lakini ujue lazima urudi kwenye maisha yako, kwahiyo acha kupoteza mda kuishi maisha yasiyokuhusu rudi kwenye mstari ishi maisha yako,
 
Mambo ya kufanya hivi sasa

1, Jitathimini hivi hayo maisha unayoishi hivi sasa ni ya kwako kweli au unaishi maisha ya mtu, maana unaweza ukakute matatizo hayakuishi mpaka inafika mahali unamsingizia shetani kuwa ndiyo sababu ya matatizo yako hayo kumbe umesahau kuwa maisha hayo unayoishi ni ya mtu mwingine wewe hauyawezi na ndio maana yanakusumbua kila siku,
 
2, hivi ni kweli hayo unayoyafanya hivi sasa ndio malengo na ndoto ya Maisha yako ya siku zote? Maana usije ukafurahia mafanikio unayoyapata hivi sasa halafu baadae ikatokea changamoto ukashindwa kuikabili na kujikuta unarudi sehemu usiyotegemea, kwasababu utakuwa unaishi Maisha ya mtu mwingine lakini ujue kunasiku utajikuta unarudi kwenye Maisha yako, kwahiyo ili hayo yote yasije yakakupata na ukaisi umeikosea Dunia basi haunabudi kwanzia sasa kujitathimini Kama unaishi Maisha yako au unaishi Maisha yasiyo yako,
 
Kama umeona unaishi Maisha yako basi haunabudi kujipongeza sana kwa nidhamu hiyo ya kuishi maisha yako, na uendelee kuboresha vyema ili yawe kiooo kwa kila anayeyatazama, Na kama umeona Maisha unayoishi sio yako kabisaaa, kwanza jitafakari upya kumbuka njia yako na urudi haraka sana maana bado haujachelewa unaweza ukarudi kuishi maisha yako na yakawa bora zaidi ya hayo yasiyoyako,hata kama unaona maisha ya mwingine ni mazuri zaidi hauna haja ya kutamani kuishi vile ujue na wewe unamaisha yako ukiyasimamia bora na kuyaboresha yatakuwa mazuri kuliko hayo unayotamani, ujue hata huyo unayetamani maisha yake alifanya kazi kubwa sana mpaka hapo yalipofikia, IGA KUTAFUTA USIIGE MATUMIZI,
 
Tukamuangalie mchawi wa biashara yako ni nani, wafanyabiashara wengi wakiona biashara zao zinaanza kuwa ngumu kitu cha kwanza huwa wanamtafuta mchawi wa biashara zao ni nani? Maana wanashindwa kuelewa kwanini jana walikuwa na wateja kibao leo wote hawawaoni tena,
Kwa wewe mwenye mawazo hayo ningeomba nikusaidie kukuonesha mchawi wako,
 
Wewe unabiashara yako na unawateja wako ambao kila siku lazima wafike kwenye biashara yako, lakini siku akija kukopa unamkatalia Kata kata,biashara yako unafungua saa moja mara saa tatu na ukiulizwa unajibu unavyojisikia na kufunga unafunga saa 11 ukiulizwa unasema unamambo mengi, ukiamua utafungua na ukiamua unafunga bidhaa zako unauza bei ya juu kuliko, unafanya yote hayo eti kwasababu eneo hilo biashara hiyo unafanya wewe tu hauna mpinzani eneo hilo,
 
Ghafla anatokea mfanyabiashara mwingine anafungua eneo hilohilo na biashara hiyohiyo na anauza bei ya kawaida, anafungua saa kumi na mbili asubuhi na anafunga saanne usiku na siku asipo fungua akijakufungua anawaomba radhi wateja wake na mteja akitaka kukopa anamkopesha bila tatizo lolote,
Kama wewe mfanyabiashara unatabia hata moja wapo hapo basi bila shaka ushamjua mchawi wa biashara yako ni nani,
 
Ushauri wangu kwa wafanyabiashara wote,
Ukiona biashara yako imeanza kuyumba usianze kumnyoshea mtu kidole, anza kujinyoshea wewe kwanza,angalia ni kipi kinasababisha wateja wako kila siku kuhama ni kwanini mteja akija kwako mara moja harudi tena, lakini ukianza kuwanyoshea watu vidole na kutafuta mchawi wa biashara yako ni nani, utafanya biashara kila sehemu hata siku moja hautowahi kufanikiwa, maana kila sehemu utahisi kunawachawi,
Bila kujijua kuwa mchawi ni wewe mwenyewe na kujirekebisha hautoendelea hata siku moja na biashara utaiona chungu na hautoitamani tena,
 
Tumefika sehemu mpaka tunamkufuru Mungu kwa kulalamika kila leo, kila siku wewe unajiona ni mtu mwenye bahati mbaya tu, hakuna siku ambayo unaiona inauhafadhali kwako, kila kitu unachokifanya unaona kama unakosea kwasababu unaona mambo hayaendi kabisa kila unalofanya halifanikiwi, kila unalolianza lazima liishie njiani, inafika sehemu mpaka unajilaani mwenyewe na kujipa majina ya ajabu, pasipokujua hayo yote wewe ndiye unayoyasababisha yatokee na yabaki yakikusumbua siku zote mpaka unahisi dunia imekukasilikia,
 
Wewe ndiyo sababu ya hayo yote yanayokutesa na kukunyima raha sikuzote, Nikwasababu hautaki kuamua ila unataka kuamliwa na wengine,
Umepata wazo la biashara ya dagaa unaenda kumshirikisha mtu ili akupe uzoefu anakwambia hiyo sio biashara kabisaa, na ukiifanya utatokea sehemu mbaya kunarafiki yangu aliwahi kuifanya na ikamuangusha vibaya sana labda ungefanya biashara ya mihogo hiyo itakutoa, basi nawewe unaondoka na maamuzi ya mtu bila hata kutafakari na kuchanganua kuwa huyo rafiki yake kama alianguka vibaya ilikuwaje labda hakuwa makini na biashara hiyo au hakuielewa vizuri, unaacha kutaka kuyajua yote hayo ila kwasababu mtu kakuamlia basi unaachana na biashara ya dagaa unaenda kuanzisha biashara ya mihogo, miezi mitatu biashara ishakwama unaanza kulalamika na kumuona Mungu kakutenga,
 
Back
Top Bottom