Ushauri wangu kwa wafanyabiashara wote,
Ukiona biashara yako imeanza kuyumba usianze kumnyoshea mtu kidole, anza kujinyoshea wewe kwanza,angalia ni kipi kinasababisha wateja wako kila siku kuhama ni kwanini mteja akija kwako mara moja harudi tena, lakini ukianza kuwanyoshea watu vidole na kutafuta mchawi wa biashara yako ni nani, utafanya biashara kila sehemu hata siku moja hautowahi kufanikiwa, maana kila sehemu utahisi kunawachawi,
Bila kujijua kuwa mchawi ni wewe mwenyewe na kujirekebisha hautoendelea hata siku moja na biashara utaiona chungu na hautoitamani tena,