Makamu mwenyekiti, ambaye ndiye mwenye uamuzi wa mwisho kuhusu kocha mpya, Ed Woodward Jumapili iliyopita aliingia kwenye vyumba vya kubadilishia huko Wembley kwenda kumpongeza Solskjaer baada ya kikosi hicho kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Tottenham Hotspur.
Na sasa Solskjaer yupo nafasi kubwa ya kupewa kibarua cha kudumu, huku kocha pekee anayemnyima usingizi kwenye kukikamatia kibarua hicho ni Mauricio Pochettino wa Tottenham Hotspur.
Solskjaer amepewa kibarua cha kuinoa Man United kwa muda hadi mwisho wa msimu, lakini baada ya kushinda mechi zote sita alizosimamia timu hiyo, upepo umegeuka na sasa kocha huyo anapendwa kuanzia kwa wachezaji, mashabiki na sasa mabosi kwenye bodi.
Ushindi huo kwenye mechi dhidi ya Spurs umeifanya United kulingana pointi na Arsenal katika mbio za kukamatia nafasi ya nne ili kufuzu kwa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Ole ameichukua United kutoka kwa Jose Mourinho.
.SUPASTAA wa Liverpool, Sadio Mane amewaambia wapinzani wao kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England, Manchester City tena kwa msisitizo: “Safari hii hatutelezi.”
Mane ana uhakika mkubwa kwamba Liverpool itabeba ubingwa wa Ligi Kuu England kwa mara ya kwanza na kukwepa kile kilichotokea misimu michache iliyopita, ambapo Steven Gerrard aliteleza na kwenye mechi ya Chelsea na kuwafanya Man City kubeba ubingwa mwaka 2014.
Kwa sasa Liverpool wapo mbele kwa pointi nne dhidi ya Man City na Mane anaamini kilichotokea huko nyuma watakuwa wameelewa somo, hivyo huu ni wakati wao wa kufanya kweli na kumaliza kiu yao ya miaka 29 ya kubeba ubingwa huo.
Mane alisema: “Hii sio timu ya watu wa kuharibu. Ubingwa tunachukua.” Tangu tukio la Gerrard limewafanya Liverpool kuwa kituko kwenye mbio za ubingwa ambapo mashabiki wengi wamekuwa wakiamini kwamba hawana uwezo wa kunyakua ubingwa huo, lazima watateleza tu kabla ya msimu kufika mwisho.
Lakini, hilo halipo kwenye akili ya staa huyo wa kimataifa wa Senegal, akisisitiza: “Nina hakika tutakuwa mabingwa wa England. Kila nikiamka, nikienda mazoezini huwa nakuwa na mawazo hayo.”
KOCHA Mkuu wa Barcelona, Ernesto Valverde ameamua kufunguka kuhusu ishu ya Neymar kwamba anapiga debe la kutaka kurudi kwenye timu hiyo yenye maskani yake huko Nou Camp.
Kocha Valverde alisema kwanza kitu kama hicho hakipo, kisha jambo jingine ni kwamba Neymar ni mchezaji wa timu nyingine kwa sasa, hivyo si jambo zuri kumzungumzia.
Kocha huyo alisema uamuzi wa Neymar kuachana na Barcelona aliufanya mwenyewe, hakuna aliyemshinikiza kufanya hivyo. Staa huyo wa Kibrazili alikwenda kujiunga na Paris Saint-Germain miaka miwili iliyopita kwa ada iliyoweka rekodi ya dunia ya karibu Pauni 200 milioni.
Lakini, maisha yake yameshindwa kubamba huko Ufaransa na sasa anapiga hesabu za kurudi kwenye La Liga, kwenda kujiunga na timu yake ya zamani. Taarifa za kutoka Hispania zinafichua kwamba baba yake Neymar amekuwa kwenye wakati mgumu na mabosi wa Nou Camp juu ya mpango wa kukamilisha dili hilo la kumrudisha mwanaye Nou Camp.
Hatuwezi kuwazungumzia wachezaji wenye mikataba na klabu nyingine, kwa wakati ule aliamua kuachana na Barcelona, basi pale ndipo ulipokoma uhusiano wetu na yeye.”