Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

KILA timu yenye kikosi matata cha kwanza kuna wachezaji hao wanaoanzia benchi, wanapoingia wanakuwa habari nyingine. Ukweli ni kwamba wachezaji hao si kama hawana uwezo ndio maana wanaanzia benchi, la viwango vyao ni vikubwa, sema kocha ni lazima awe na kikosi chake cha kwanza anachoanza nacho.
 
Kwenye Ligi Kuu England wapo wachezaji hao wanaoanzia benchi na kila wanapoingia uwanjani, basi wamekuwa wakifanya mambo makubwa kusaidia timu zao.
 
5. Romelu Lukaku

(Mechi 7, mabao 3)

Straika wa Manchester United, Romelu Lukaku amekuwa akipambana kuweka sawa kiwango chake cha soka kwa msimu huu baada ya mambo kuwa magumu upande wake. Kutokana na hilo, Lukaku amejikuta akiishia kwenye benchi mara kadhaa. Lakini, mara zote alizotokea benchi, Lukaku alijaribu kuonyesha yeye ni matata baada ya kuhusika kwenye mabao matatu.
 
Amekuwa na kiwango bora, lakini Kocha Mauricio Pochettino amekuwa akipendelea zaidi kumwaanzishia kwenye benchi. Kwenye Ligi Kuu England msimu huu ameanzishwa mara saba tu, huku mechi saba akitokea kwenye benchi na kuhusika katika mabao manne.
 
3. Xherdan Shaqiri

(Mechi 7, mabao 4)

Wakati anasajiliwa na Liverpool, Xherdan Shaqiri alionekana kama mzigo tu, lakini baada ya ligi hiyo kuchezwa kwa mechi 23, fowadi huyo wa kimataifa wa Uswisi amethibitisha ni mmoja kati ya usajili bora kabisa uliofanywa na Kocha Jurgen Klopp.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…