Bingwa mara nane wa Olimpiki Usain Bolt ametangaza kuwa "maisha yake ya michezo yameisha", baada ya kushindwa kuanza maisha rasmi ya soka la ushindani baada ya kung'ara kwenye riadha.
Bolt, raia wa Jamaica, 32, alikuwa akijinoa na kwa miezi miwili nchini Australia na klabu ya Central Coast Mariners, lakini akaondoka mwezi Novemba baada ya klabu hiyo kushindwa kupata fedha za kumsajili.
"Ilikuwa ni furaha kwa kadri ilivyodumu," amsema Bolt ambaye bado anashikilia rekodi za dunia kwenye mbio fupi za mita 100 na 200. "Sitaki kusema kuwa hatukuliendea suala hili kama vile ilivyotakiwa, na naamini tulifanya kila ambacho tulitakiwa kufanya kwa namna sahihi."