Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Maisha ya chui kwa kiasi flani hufanana na maisha ya mwanadamu, hasa wale ambao hukulia mitaani kwa kutelekezwa na wazazi, kwani miezi mitatu tuu baada ya mtoto wa chui kupata kuona mama yake huanza kufanya majaribio ya kutaka kumtoroka, na yote hiyo huwa ni sehemu ya kumuona mwanaye anawezaje kujitegemea pasina wazazi wake, siku ambayo atafanikiwa tuu kupanda juu ya mti ndio siku ambayo hatamuona tena mama yake.
 
Kimsingi kuna aina nyingi za chui, lakini hapa kwetu bongo chui aina zote huwa tunaita chui, wenzentu wazungu wamewagawa chui katika makundi na majina yake mfano kuna 1. Tiger huyu ni chui ambaye huwa na mistari mweupe, 2. Jaguar huyu ni chui mweusi kibongo bongo tunasema duma. 3. Cheetah huyu ni mwembamba na mrefu sana.
 
Hao ni baadhi tuu ya chui lakini bado kuna aina nyingine nyingi za chui, na pia kama ulikusa hujui hapa kwetu bongo baadhi ya chui hatuna ikiwa ni pamoja na Tiger, chui waishio katika barafu nk.
 
Chui ni kiumbe ambaye huwa na uzito wa kg 30 mpaka 100 na ushee, uzito wake hutegemea umri, jinsia na afya, huzaa watoto wawili mpaka wanne, watoto wake huvutia sana wanapokuwa na miezi kadhaa, anaweza kukushawishi umbebe japokuwa utata ni toka utotoni !
 
Muda mwingi wawapo katika umri huo mama zao hupenda kujificha ili kuwapa nafasi ya kuanza kujitegemea mapema, lakini atokeapo mnyama wa ajabu mbele yao, mtoto wake akiunguruma tuu mama yake hutokea ndani ya sekunde chache utafikiri kasafirishwa na umeme, na yoyote anayekutwa eneo hilo ni lazima ajutie uwepo wake eneo hilo.
Chui watoto huanza kujitegemea mapema sana, hivyo chakula chao huwa nyoka, wadudu, panya, nyani, sungura, samaki nk.
 
Mnyama huyu haamini katika kitu kinaitwa familia, ndio tofauti yake kubwa na wanyama wengine, hapendi mapenzi ya kugandana, ni kawaida sana kukuta dume lipo lenyewe na jike kivyake, kutokana na tabia hiyo chui ni mnyama mwenye tabia ya kuhonga sana kwa majike,
 
anapopata msosi safi lazima mwingine akaweke akiba katika makazi yake special kwa jike mzuri kwake siku hiyo, japokuwa hata majike yana uwezo mzuri wa kuwinda ila wao si mafundi sana Kama yalivyo madume kwahiyo madume hutumia nafasi hiyo kuwanasa warembo, na jike anapopata mimba hiyo ni gharama ambayo huibeba peke yake, dume halihusiki tena, na katika kipindi hicho hukaa wiki moja tuu kabla dume halijatoa taraka, jike huamua kuondoka mwenyewe.
 
Chui pia huishi katika maeneo ambayo hujimilikisha wao wenyewe, mipaka yao huweka alama kwa mikojo yao, ni mlinzi ambaye hapendi mchezo kwenye mipaka yake.
 
VYAKULA APENDAVYO*******
Chui hula mnyama alaye nyama tuu vyakula vyake ni pamoja na Paa, nyani, mbawala, sungula, mbuni, twiga, samaki nk.
Pamoja kwamba Twiga ni mnyama anayeogopwa hata na simba lakini chui humkamata jamaa huyu kiurahisi pindi afatapo majani ya juu, chui hukamata shingo yake na kumshusha chini mpaka atakapomuua.
 
WANYAMA WAMSUMBUAO KUWAWINDA*******
Chui hupata shida sana kuwawinda wanyama wenye kila nyingi, kama nyati, pundamilia, nyumbu nk, na hii ni kwa sababu ya uzito wake kuwa mdogo sana ukifananisha na uzito wa wanyama hao, lakini anapofanikiwa kumkamata shingo tuu huwa hamuaachii mpaka kieleweke, na hii ndiyo nafasi ambayo madume hutumia kuwapata majike, kwani chui dume uzito wake ni mkubwa zaidi ya jike, hivyo wanyama wenye kilo nyingi madume ndio huwa mstari wa mbele.
Chui wakikutana katika windo moja hawana shida, wakikamata wanagawana na wakati mwingine hutafutana kushirikiana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…